Hatimaye wapenzi wa kisakuzi cha UC Browser sasa wanaweza kuendelea kufurahia kisakuzi hicho mara baada ya kurudishwa kwenye soko la Play Store.
Kisakuzi hicho kilitolewa na Google kutoka kwenye soko la Play Store siku chache zilizopita, huku kikiwa kinashutumia kwa makosa mbalimbali ikiwa pamoja na ile ya kuwa kisakuzi hicho hutuma data za watumiaji wake bila ruhusa kwenda nchini china pamoja na kuvunja sheria za soko la Play Store
Aidha pamoja na hayo wahusika wa kisakuzi hicho kutoka kampuni ya UC Union, wiki hii walitangaza kuwa sababu za kuondolewa kwa kisakuzi hicho ni kutokana na aina fulani za mpangilio (settings) zilizokuwa ndani ya programu hiyo zilikua haziendani na vigezo na masharti ya google kupitia soko lake la Play Store.
Hata hivyo kampuni hiyo ilikanusha kuhusu tuhuma za kisakuzi hicho kutuma data za watumiaji wake nchini china huku msemaji wa kampuni hiyo akiwataka watumiaji wake kuendelea kufurahia matumizi ya kisakuzi hicho ambacho sasa kimerejea kwenye soko la Play Store.
Kisakuzi cha UC Browser sio maarufu sana kwa watumiaji wengi wa Android kutokana na simu hizo kuja na kisakuzi cha Google Chrome mara baada ya kununua simu hizo, lakini hata hivyo kisakuzi hicho kimejizolea umaarufu mkubwa kwa nchini india pamoja na china.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.
Maoni* napenda kuwa pamoja na nyie