Mara baada ya tetesi za muda mrefu juu ya ujio wa Infinix ZERO 8, hatimaye kampuni ya simu ya Infinix kupitia mitandao yake ya kijamii @infinixmobiletz wameitambulisha rasmi Infinix ZERO 8.
Kwa mujibu wa kampuni ya Infinix, Infinix ZERO ndio kinara ‘flagship model’ kwa mwaka huu wa 2020 na ikiwa kama simu yenye kuiwakilisha kampuni ya Infinix, Infinix ZERO 8 imebeba sifa lukuki kama zifuatazo;
Simu hii inakuja na MTK Helio G90T processor, RAM ya GB 8 ROM ya GB 128, vyote vikiwa vinaifaya Infinix ZERO 8 kuwa na ufanisi zaidi wa kufungua kubeba files, videos na games zenye ukubwa wa aina yoyote pasipo kugoma goma. Vile vile Infinix ZERO 8 ina teknolojia ya 3D ambayo hii ni maalumu kwa ajili ya kupunguza joto la simu endapo utaitumia simu yako kwa muda mrefu.
Infinix ZERO 8 ina kamera zenye kubeba megapixel kubwa, nyuma ikiwa ni Megapixel 64 selfie ikiwani Megapixel 48, kamera hizo zimetengenezwa kwa sensor ya IMX686 Sensor ambayo ni maalumu kwa ajili ya kupiga picha kali na zenye uhalisia pasipo kujali muda wala mazingira.
Infinix ZERO 8 inauwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya siku moja kutokana na matumizi yako, huku uwezo wake mkubwa wa battery ya 4500 mAh ukikuwezesha kutumia simu hiyo bila wasiwasi, mbali na hayo simu hii inakuja na teknolojia ya Fast Charging 33W Super yenye uwezo wa kufanya simu hii kujaa chaji kwa haraka ndani ya muda mfupi.
Muonekano wa Infinix ZERO 8 ni premium, na ukweli naweza kusema simu hii inakuja na desgin ya kuvutia sana kutokana na muundo wake kuwa mwembamba na wigo mpana wa kioo cha inch 6.85 FHD+.
Kwa sasa Infinix ZERO 8 ipo Tanzania na unaweza kuipata katika maduka yote ya simu kwa bei isiyozidi Tsh.750,000/=