Hatimaye Pope Francis Kuanza kutumia Instagram

Hatimaye Pope Francis Kuanza kutumia Instagram Hatimaye Pope Francis Kuanza kutumia Instagram

Mitandao ya kijamii kwa sasa ni kitu ambacho akikwepeki kwa baadhi ya watu duniani iwe mfanya biashara, mtu maarufu au hata wewe binafsi kuwa na social network ni kitu cha ulazima sana hasa kwenye ulimwengu wa leo wa sayansi na technolojia. Kipindi cha nyuma kidogo kuwa na social media network au mitandao ya kijamii ilikua ikionekana kama ni chaguo la mtu tu, lakini sasa ilikupata taarifa pamoja na mambo mengine ya msingi ni lazima uwe na mitandao hii ya kijamii ambayo kwa sasa ni gumzo sana duniani kote.

Moja kati ya mitandao ambayo ni gumzo sana kwa sasa duniani ni mtandao wa kijamii wa Instagram mtandao huu kwa sasa una watu zaidi ya milioni 400 pamoja na kuwa na watumiaji zaidi ya milion 75 kila siku, kwa kuwa moja kati ya mtandao ambao ni maarufu sana duniani watu wengi maarufu wameonekana kujiunga na mtandao huo ili kujichanganya na watu mbalimbali wanao wapenda duniani.

Advertisement

Hivi karibuni Pope  Francis wa 226 alitoa taarifa za kujiunga na mtandao huo, kupitia redio ya vactican Pope Francis ambae ni kiongozi wa kanisa katoliki alisema kuwa atajiunga na instagram siku ya tarehe 20 March 2016 kwa kutumia jina la “franciscus”. Taarifa hizi zilisambaa kote duniani hadi kufikia tarehe ya jana yani 20 March Pope huyo alipojiunga na instagram account yake hiyo ilikua na follower zaidi ya 1.5m ikiwa na picha tano tu.

https://www.instagram.com/p/BDIgGXqAQsq/?taken-by=franciscus

Post hii ndio picha ya kwanza ya Pope Francis baada ya kujiunga na instagram hapo jana siku ya tarehe 20 March 2016. Hii ni mara ya pili kwa pope francis kujiusisha na mitandao ya kijamii baada ya kutumia mtandao wa kijamii wa twitter kwa miaka mitatu sasa kuanzia account hiyo ilipo anzishwa tarehe 23 February 2012 na Pope Benedict XVI na baadae Pope Francis alipojiunga na mtandao huo tarehe 17 March 2013 kwa kutumia jina la hilo hilo la “@Pontifex”.

Pope Francis ni pope wa pili baada ya Pope Benedict XVI kuanza kutumia mitandao ya kijamii. Hii inaonyesha umuimu wa kuwa na mitandao ya kijamii kwa sasa kwenye dunia hii ya sayansi na technolojia.

Kama bado hauna Application ya instagram na Twitter kwenye smartphone yako na unatumia iOS.?  Pakua hapa Application hizo na uanze kuwafuatilia watu maarufu duniani akiwemo Pope Francis wa 226.

[appstore id=389801252] [appstore id=333903271]

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use