Hatimaye kampuni ya Apple hapo jana imetangaza rasmi kuwa, sasa App ya shazam pamoja na teknolojia yake ipo chini ya kampuni ya Apple.
Baada ya Taarifa za kuhusu ununuzi huo, Apple ilitangaza rasmi kununua App hiyo hapo jana na inasemekana kuwa Apple imetoa kiasi cha dollar za marekani milioni 400 ingawa bado hakuna taarifa kamili kuhusu kiasi hicho.
Hata hivyo ripoti kutoka kwenye tovuti ya Tech Crunch zinasema kuwa Apple ilikuwa kwenye mazungumzo ya kununua App hiyo miezi mitano iliyopita wakati kampuni za Snapchat na Spotify nazo pia kwa wakati huo zilikuwa kwenye mazungumzo ya kutaka kununua App hiyo.
Kwa sasa wafanyakazi wa kampuni ya Shazam pamoja na teknolojia nzima ya kampuni hiyo wote wako chini ya kampuni ya Apple kwa kiasi cha dollar za marekani milioni 400 sawa na shilingi za kitanzania Tsh Bilioni 890.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.