Raisi wa Tanzania Azindua Rasmi Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki

Unaweza kupata hati hizo mpya kwa kutuma maombi kupitia mtandao
Hati mpya ya kusafiria ya Kielektroniki Tanzania Hati mpya ya kusafiria ya Kielektroniki Tanzania

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh John Pombe Magufuli hivi leo amezindua rasmi hati mpya ya kusafiria ya kielektroniki au e-passport sambamba na mfumo mpya wa uhamiaji kupitia mtandao au e-migration.

Mfumo huo mpya wa (e-migration) umezinduliwa rasmi leo huku idara ya uhamiaji ikianza na awamu ya kwanza ya utoaji wa passport au hati za kielektroniki maarufu kama e-passport. Hati hizo zitakuwa na ulinzi zaidi na zitakuwa na uwezo wa kunganishwa na idara mbalimbali za serikali kwa njia ya mtandao kama vile mamlaka ya mapato ya Tanzania (TRA), mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), Polisi (Interpol) pamoja na mamlaka nyingine za ndani ya serikali ya Tanzania.

Advertisement

Hati hiyo mpya ya kielektroniki imetengenezwa na kampuni maarufu ya marekani ya kutengeneza bidhaa za ulinzi inayoitwa HID Global, Hata hivyo kwa mujibu wa mwakilishi wa kampuni hiyo aliyekwepo kwenye uzinduzi huo hati hiyo itakuwa na ulinzi mkubwa na itawawezesha wasafiri kuweza kuwa na copy au nakala ya hati hiyo kwenye simu ya mkononi baada ya kupakua app maalum ya e-passport na hii itasaidia zaidi pale passport hiyo itakapo potea.

Akizungumzia juu ya utoaji wa Hati hiyo mpya, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala, amesema kuwa hati hizo mpya za kieletroniki zitakuwa zinapatikana kwa kutumia kitambulisho cha Taifa kama sharti muhimu na zita patikana kwa gharama ya shilingi za kitanzania Laki moja na nusu (150,000) kwa muda wa miaka 10 ambayo ni sawa na shilingi 15,000 kwa mwaka. Hata hivyo passport hizo mpya zita patikana pia kwa kutuma maombi kupitia mtandao.

Kuhusu passport za zamani, kamishna hyo libainisha kuwa passport za zamani ambazo ndio zinatumika sasa zitaendelea kutumika hadi hapo ifikapo mwezi January mwaka 2020 ambapo wananchi wote wanao tumia passport za zamani wanatakiwa kuwa na passport hizo mpya za kielektroniki au e-passport.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use