Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Video : Harusi ya Prince Harry Kuonyeshwa Mubashara YouTube

Hakuna haja ya TV sasa mambo yote ni YouTube
Harusi ya Prince harry Harusi ya Prince harry

Kama wewe upo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii nadhani lazima utakuwa unajua kuwa kesho ndio ile harusi kubwa kuliko zote inayo muhusu Prince Harry, mtoto wa mwisho wa Charles, Prince of Wales kutoka familia ya malkia Elizabeth.

Harusi hiyo inatarajiwa kuuzuriwa na Malkia Elizabeth, pamoja na watu wengine maarufu mbalimbali kutoka nchi mbalimbali. Hata hivyo harusi hiyo inatarajia kurushwa mubashara kabisa na vituo vya televisheni kutoka ndani na nje ya nchi ya england na kwa sababu teknolojia inazidi kukuwa kwa kasi sana siku hizi, hapo siku ya kesho utaweza pia kushuhudia harusi hiyo ya kifalme moja kwa moja mubashara kabisa kupitia mtandao wa YouTube.

Advertisement

Harusi hiyo itarushwa mubashara kwenye channel ya YouTube The Royal Family, ambayo inategemewa kuonyesha matukio yote ya muhimu kuanzia kanisani, mpaka kwenye hafla ya harusi hiyo itakayo fanyika kwenye kasri ya kifalme ya Windsor Castle. Matangazo hayo yanategemewa kuanza kesho siku ya jumamosi ya tarehe 19, saa saba mchana kwa saa za Afrika ya mashariki.

Bila kusahau kwa wale wapenzi wa mpira wa miguu, YouTube pia itaonyesha mchezo wa fainali ya uefa champion league kati ya Liverpool na Real Madrid, siku ya tarehe 26 mwezi huu wa Tano.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use