Ikiwa na watu milioni 29.8, au karibu nusu ya idadi ya watu wa Tanzania, wanaojiunga na huduma za mtandao, utafiti mpya unaonyesha kuwa Halotel ina mtandao wa simu wa kasi zaidi nchini.
Ookla, ambayo inamiliki na kuendesha huduma ya kupima kasi ya mtandao maarufu ya speedtest.net, imechapisha viwango vyake vya hivi karibuni vya Speedtest Global Index kwa Tanzania kwa robo ya kwanza ya 2022, ambayo inaonyesha kuwa Halotel imezizidi kampuni kubwa za mawasiliano kama Vodacom Tanzania na Airtel kwenye simu.
Halotel imeonekana kuwa na kasi ya upakuaji (Download) wa wastani wa kasi ya Megabytes 17.84 kwa sekunde (Mbps) ikifuatiwa na Vodacom (12.09 Mbps), Airtel (10.6 Mbps), TTCL (10.4 Mbps).
Tigo Tanzania na kampuni dada yake Zantel ikiwa na kasi ya upakuaji ya wastani ya 5.99 Mbps na 4.31 Mbps kwa Zantel.
Halotel pia ilipata Alama ya juu kabisa ya Uthabiti, ya asilimia 80.1, mbele ya Vodacom iliyoshika nafasi ya pili kwa asilimia 72.1. Alama hii inaonyesha asilimia ya matokeo ya majaribio ya kasi ambayo yalifikia kasi ya upakuaji (Download) angalau 5Mbit/s na kasi ya upakiaji (Upload) angalau 1Mbit/s.
TTCL ina asilimia 67.5, Airtel asilimia 67.2, wakati Tigo na Zantel zikiwa na asilimia 48.9 na 37.4.
Speedtest Global Index inalinganisha data ya kasi ya mtandao kutoka kote ulimwenguni kila mwezi. Data hizo hutoka kwa mamilioni ya majaribio yanayochukuliwa na watu halisi wanaotumia Speedtest kila mwezi.
Hata hivyo zipo sababu nyingi zinzoweza kuchangia kuongezeka au kupungua kwa speed ya Internet kwenye mtandao husika, moja ikiwa ni pamoja na eneo mtumiaji alilopo pamoja na aina ya kifaa anachotumia.
Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata internet ya kasi kwenye maeneo ya mbali hasa maeneo ya vijijini.
ni kweli