Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Game ya Halo Wars 2 Yazinduliwa Kwenye Xbox na Windows 10

Baada ya kusubiri kwa muda sasa Halo Wars 2 hii hapa..
Halo Wars 2 Halo Wars 2

Kwa wale wapenzi wa video game hapo jana kampuni ya Microsft ilifanya uzinduzi rasmi wa game ya Halo Wars 2, Game hii ni mfululizo wa misimu saba ya Game za Halo na msimu huu unatokea kwenye mfululizo wa msimu wa game ya Halo Wars iliyozinduliwa mwaka 2009.

Kuhusu stori ya game ya Halo Wars 2, hivi sasa kwenye msimu huu game hii ina anzia miaka 2559,28 baada ya kutokea vita vya Halo maarufu kama Halo Wars, Captain Cutter na kikosi chake wanakutana na kikwazo kipya cha kupambana na maadui wajulikanao kama the Banished huku waki ongozwa na kiongozi wao anaeitwa Atriox. Vita ni vinatokea huku Captain Cutter akijitahidi kuponya uhai wa kikosi chake kutoka kwenye mikono ya kikundi cha magaidi cha The Banished.

Advertisement

Game hii imewezeshwa kuchezwa kwa aina mbili yani Single Player na Multiplayer, kuhusu bei Halo Wars 2 inapatikana kwenye Xbox na Windows 10 kwa dollar za marekani $59.99 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 150,000 kwa hapa Tanzania. Unaweza kuangalia list ya game nyingine na tarehe ya kutoka kupitia hapa Tanzania Tech.

Kwa habari zaidi za game na nyingine nyingi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku au pakua app ya Tanzania Tech kupitia Play Store, pia kuna teknolojia nyingi za kushangaza ambazo ulikua uzijui ili kuzijua ungana na channel yetu kupitia Youtube ili kupata habari kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use