Hapo jana watu wasiojulikana walifanya shambulizi la DDoS kwenye kituo kinacho husika na usambazaji wa haraka wa baadhi ya tovuti kubwa duniani, kituo hicho cha DynDNS hushulika na kufanya upatikanaji wa baadhi ya tovuti kubwa duniani kama vile Amazon, Netflix, Reddit, Paypal, Twitter na nyingine kuwa wa urahisi na wa haraka kwa kutumia Server za kituo hicho.
Kama unajiuliza shambulizi la DDos ni nini..? kwa kifupi ni kwamba DDoS kirefu chake ni Distributed Denial of Service hii ni aina ya shambulizi ambalo hufanywa na kikundi cha watu ambapo hapa IP addresses zaidi ya milioni hutumiaka ili kufanya server za kituo cha usambazaji wa tovuti flani kufurika na kushindwa kufanya kazi kwa watu wanaotaka kutumia tovuti hizo. Kwa kuelewa zaidi shambulizi la DDoS ni kama vile watu wengi waliojazana ndani ya ofisi flani na kutokana na wingi wa watu hao husababisha watu wengine kushindwa kuingia kwenye ofisi hizo.
Hata hivyo kituo hicho cha usambazaji cha DynDNS kilishambuliwa na shambulizi hilo mara tatu kiasi cha polisi wa usalama wa nchini marekani FBI kuanza kufanya uchunguzi wa nani anae husika na shambulizi hilo. Kwa hapa Tanzania jana usiku mida ya saa nne mpaka saa sita usiku tovuti maarufu kama vile Twitter, Amazon pamoja na Reddit zilikua zikisumbua katika upatikanaji wake.
Mpaka sasa bado hakuna mtu yoyote au kundi la hackers ambao limetangaza kuwa linahusika na shambulizi hilo. kwa habari zaidi kuhusiana na shambulizi hili endele kutembelea tovuti ya Tanzania tech kwani tutakuwa tukiendelea kuwaletea muendelezo wa habari hii.
Kama unataka kupata habari hizi na nyingine nyingi unaweza kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram bila kusahau Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.
Oky Thank you Jasmine