Habari na karibu kwenye makala nyingine ya Techwiki, kupitia kipengele hichi tumeku kukusanyia habari zote za teknolojia ambazo pia ni muhimu ambazo zimejiri kwa wiki nzima inayo anzia siku ya jumapili hadi siku ya jumamosi. Miongoni mwa habari tulizo nazo wiki hii ni pamoja na
TABLE OF CONTENTS
Kampuni ya TECNO Yashutumiwa Kuuza Simu Zenye Malware Barani Africa
Kwa mujibu wa tovuti ya CNN Business, kampuni ya TECNO inashutumiwa kuuza simu barani Africa, ambazo zina semekana kuwa na programu haribifu (Malware) ambayo inayokula data za watumiaji na kusajili watumiaji kwenye huduma zisizo hitajika, programu hiyo imepatikana ikiwa imewekwa kabla ya simu hizo kuuzwa (Pre-Installed) kwenye maelfu ya simu za bei nafuu zilizo uzwa barani Afrika zaidi ya miaka miwili baada ya kugunduliwa kwa tatizo hilo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, programu hiyo haribifu (Malware) inayoitwa Triada malware, huwa na tabia ya kuunganisha watumiaji wa simu kwenye vifurushi vya kulipa bila wateja kujua na bila ruhusa yao, imepatikana kwenye simu za TECNO W2 kwenye nchi za Africa kama vile Ethiopia, Ghana, Cameroon na Afrika Kusini.
CNN Business imeandika kuwa, Secure-D ambalo ni jukwaa la kupambana na ulaghai ambalo lilifanya utafiti huo, lilirekodi miamala milioni 19.2 ya tuhuma tangu Machi 2019 kutoka zaidi ya vifaa 200,000 vya kipekee.
Katika taarifa kwa CNN Business, TECNO Mobile ilisema hii ” ilikuwa shida ya usalama ya zamani na iliyosuluhishwa kwa watumiaji wote ulimwenguni” tatizo hilo lilipatiwa suluhisho mnamo Machi 2018. Wateja wanaopata shida kwa sasa wanapaswa kupakua sasisho kupitia simu zao au wanaweza kuwasiliana na watoa huduma wa mauzo kwa msaada zaidi, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok Ajiuzulu
Wakati mtandao wa TikTok ukiendelea kupitia hali ngumu, hivi karibuni taarifa zinasema kuwa aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya TikTok Kevin Mayer, ametangaza kujiudhulu rasmi huku akieleza sababu ni machafuko ya kisiasa yanayoendelea kati ya China na Marekani.
Miezi Michache iliyopita, kampuni ya TikTok ilimuajiri Kevin Mayer ambaye ni mwananchi wa marekani kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya hiyo TikTok ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Byte Dance ya nchini China. Hata hivyo inasemekana kuwa hii ilikuwa ni hatua ya TikTok kuonyesha umma kuwa kampuni hiyo inafaa kuaminika kwa kuajiri watu kutoka nchi mbalimbali bila kubagua.
Katika wiki chache zilizopita, TikTok imekumbwa na shinikizo kubwa kutoka kwa utawala wa Trump. Huku Trump akidai kwamba kampuni ya Amerika inunue biashara ya TikTok ya Amerika mpango ambao ni mgumu ikizingatiwa kuwa TikTok ni kampuni inayofanya kazi zake dunia nzima.
Game za Epic’s Games Kutokupatika Kwenye Mfumo wa iOS
Kama umekuwa mfuatiliaji wa maswala ya Teknolojia ni wazi unajua kuwa kampuni ya Apple ipo kwenye mgogoro mkubwa na kampuni ya Epic Games, Mgogoeo ambao wiki hii umechukua sura mpya baada ya kampuni ya Apple kufuta akaunti ya Epic’s Games na kutangaza kuwa Game za kampuni hiyo hazitokuwepo tena kwenye mfumo wa iOS.
Game za Epics Games ni pamoja na game maarufu ya Fortnite ambayo ndio ilileta mgogoro unaendelea kwa sasa, pamoja na games nyingine kama Infinity Blade na nyingine.
Kufutwa kwa akaunti hiyo kuna maana kuwa hakuna update za game hiyo kwa wale wenye game hiyo kwenye vifaa vya iOS na iPad ikiwa pamoja na kuzuiwa kwa ununuzi wa baadhi ya vitu kwenye game hiyo kama vile silaa za kigemu na nguo mbalimbali kwaajili ya game hiyo.
Kampuni ya Inifnix Imezindua Simu Mpya ya Infinix Zero 8
Kampuni ya Infinix, wikii imeingiza sokoni simu yake mpya ya Inifnix Zero 8, simu hii imezinduliwa huko nchini Indonisia huku ikitarajiwa kuzindualiwa duniani kote mapema mwezi ujao. Simu hii ni moja kati ya simu yenye uwezo mkubwa huku ikiwa na muonekano wa kipekee na wakwanza kwenye simu za Infinix.
Japokuwa kampuni ya Infinix inao utaratibu wa kutoa simu yenye sifa tofauti kwa kila nchi, simu hii ya Infinix Zero 8 inakuja na sifa nzuri sana kwa mtumiaji au mpenzi wa simu za Infinix. Simu hii inakuja na sifa zifuatazo.
- CPU: Octa-Core 2x 2.05GHz Cortex-A76 & 6x 2.0GHz Cortex-A55
- RAM: 8 GB
- Storage: 128 GB
- Display: IPS LCD, 6.85 inches
- Camera: Quad 64 MP, 8 MP, 2 MP, 2 MP
- OS: Android 10
Jeff Bezos Tajiri Pekee Duniani Mwenye Thamani ya Dollar Billion 200
Mwanzilishi na mkurugenzi mtendani wa kampuni ya Amazon, hivi karibuni amevunja rekodi kubwa ya kuwa tajiri pekee duniani ambaye amefikia thamani ya dollar bilioni 200. Jeff Bezos ambaye ana miaka 56 kwa sasa ndio mtu tajiri zaidi kuliko matajiri wote duniani huku utajiri wake ukiwa unaongezeka zaidi kadri siku zinavyo kwenda.
Jeff Bezons alianzisha tovuti ya Amazon.com katika karakana ya nyumba iliyokodisha huko Bellevue, Washington. Wazazi wa Bezos waliwekeza karibu dollar $ 250,000 katika kuanzishaji wa tovuti hiyo. Mnamo Julai 1995, tovuti hiyo ilianza huduma kama duka la vitabu. Katika miezi miwili ya kwanza ya biashara, Amazon iliuza kwa majimbo yote 50 na zaidi ya nchi 45.
Na hizo ndio habari kubwa za Teknolojia kwa wiki hii inayo ishia leo tarehe 29/08/2020. Kama wewe ni mpenzi wa Tanzania Tech hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani kuna kitu kikubwa sana kina kuja na natumaini kitaweza kusaidia watu wote hasa wapenzi wa teknolojia kuweza kutengeneza pesa mtandao kwa haraka na urahisi.
Kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita ya tarehe 22/08/2020 basi unaweza kusoma habari zote kupitia ukurasa huu. Kwa habari zaidi na maujanja mbalimbali hakikisha una jiunga nasi kwenye channel yetu ya YouTube Hapa.