Kampuni ya Google ambayo ndiyo inayomiliki uwanja au (Domain) za blogspot leo imetangza kuweka ulinzi maalumu wa HTTPS kwenye domain zake hizo, google hivi karibuni imeonakana sana kusisitiza matumizi ya ulinzi huo wa HTTPS ikisema kuwa kuna faida nyingi sana za kutumia ulinzi huo.
Kwa wale msio ijua HTTPS ni ulinzi maalumu ambao unawekwa kwenye blog ama website ili kusaidia ulinzi wa data za watumiaji wa blog yako pamoja na data za hiyo blog yako, hata hivyo kuna faida nyingi sana za kutumia HTTPS, faida ya kwanza ikiwa ni ulinzi na faida nyingine zikiwemo kutokea kwanza kwenye search engine na mengine mengi. Google ilitangaza toka mwaka 2014 kuwa inafanya mpango wa kuweka ulinzi huo kwenye domain zake zote na pia itatoa kipaumbele kwa blog au website zenye ulinzi huo maalumu wa HTTPS.
Kama wewe unatumia blogspot na bado blog yako haina ulinzi huo maalumu wa HTTPS unaweza ukafuata maelekezo haya ili kujua kama tayari blog yako imewezeshwa. Kwanza utacopy jina la blog yako kwa mfano tzhealth.blogspot.com kisha uta-paste tena hapo utaona jina la blog yako likiwa limeanza na http:// yani itakua hivi http://tzhealth.blogspot.com ongeza herufu “S” mbele ya “P” itakua hivi https://tzhealth.blogspot.com kisha bofya enter hapo utaona kuna kufuli la kijani kukiwa na herufi HTTPS. Kwa kufanya hivyo basi utakua umethibitisha kuwa blog yako inayo ulinzi wa kutosha wa HTTPS.
Hapo awali kuweka ulinzi huu ilikua sio jambo la lazima lakini saa google wameweka blogspot zote kuanzan na kiunganishi icho cha ulizni cha HTTPS hata hivyo blog za wordpress nazo zilishanza zoezi hilo toka mwaka 2014 kwanye kiunganishi chake cha wordpress.com hapo zamani ulinzi huu kwa domain ya kawaida ulikua ukichajiwa kuanzia dollar za kimarekani $100 mpaka $150 kwa mwezi lakini sasa shukurani kwa teknolojia huduma hii ni free kabisa.