Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Google Yasitisha Utengenzaji wa Simu Yake ya Project Ara

Google Imeamua kusitisha utengenezaji wa simu yake maarufu kwa jina la Project Ara
Google yaacha project Ara Google yaacha project Ara

Kampuni maarufu ya teknolojia ya Google mapema hapo jana ilitangaza kusitisha utengenezaji wa simu yake almaarufu kama project Ara, taarifa hizi zimekuja rasimi mara baada ya uvumi kuanza kusambaa kuwa kampuni hiyo imesimamisha utengenezaji wa simu hiyo. Google ilitangaza rasmi hapo jana kuwa imesitisha simu hiyo rasmi na hakutakua na mategemeo ya kuendela na utengenezaji wa simu hiyo siku za hivi karibuni.

Kwa wale ambao hawaijui simu hiyo ya Google maarufu kama Project Ara ni simu yenye uwezo wa kukuwezesha kubadilisha vifaa vya simu yako kama vile kioo, spika, ram na hata vitu vingine ambavyo kwenye simu za sasa havibadilishiki.

Advertisement

Hata hivyo taarifa hizo zimewashitua wapenzi wengi wa simu hiyo walio kuwa wanaisubiri simu hiyo kwa hamu. Hata hivyo Google hawakusema kuwa ni lini itaendelea na utengenezaji wa simu hiyo ya kisasa kutokana na kwamba Google iliangaza kuwa wamesitisha na sio wameacha utengenezaji wa simu hiyo moja kwa moja. mhhh!

Je wewe unafikiriaje..? Google wameshindwa kuendeleza Project hii kwaajili ya ugumu au wanampango wa kuja na kitu kingine kikubwa zaidi..? Andika komenti yako hapo chini…

Pia ili kujua kama google wataendelea na simu hii au wamepanga nini endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use