Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Google Yaleta App Mpya Kwaajili ya Picha (Download Hapa)

Programu mpya ya picha kutoka Kampuni ya Google hii hapa
picha picha

Google kupitia soko lake la Google Play Store leo imetambulisha programu yake mpya kwaajili ya Android, programu hiyo ambayo ilitoka awali kwenye mfumo wa iOS sasa imekuja rasmi kwenye mfumo wa Android.

Programu hiyo iliyopewa jina la Motion Stills imetengeneza na Wahandisi wa Programu za Utafiti wa Google ambao wamesema kuwa wamesikiliza maoni ya watu wengi kuhusu kuleta programu hiyo kwenye mfumo wa Android na sasa wameleta programu hiyo huku ikifanya zaidi kidogo ya ile ya mfumo wa iOS.

Advertisement

Programu hiyo mpya itakusaidia kuchukua video ya dakika chache na kuifanya irudie rudi, pia vilevile utaweza kubadili video ya kawaida kuwa kwenye mfumo wa GIF, vilevile programu hiyo ina kuruhusu kurekodi video na kuipeleka mbele kwa haraka kwa njia inayoitwa Fast Forward. Programu hiyo pia itakupa uwezo kuzuia mitetemeko mbalimbali inayotokea pale unapo piga picha hivyo hata kama una ruka juu kwa nguvu ili kupiga picha programu hiyo itaweza kuzuia mitetemeko inayotokea kwenye picha kutokana na kuruka huko juu.

Kizuri zaidi picha hizo na video hizo unaweza kutuma moja kwa moja kwa rafiki zako hata kama hana programu hiyo. Ili kuwa na programu hiyo kwenye simu yako unatakiwa kuwa na simu ya Android yenye toleo la 5 na kuendelea, unaweza kudownload programu hiyo kwa mfumo wa android na iOS kwa kubofya link hapo chini.

Motion Stills kwa Mfumo wa Android

Motion Stills
Price: Free

Motion Stills kwa Mfumo wa iOS

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : The Verge

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use