Kila mwaka kampuni ya Google imekuwa ikiwapa nafasi watumiaji wa simu za Android, pamoja na watengenezaji wa programu mbalimbali kujaribu mfumo mpya wa Android. Mwaka huu Google imekuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa majaribio wa “Android P”.
Sasa ikiwa bado mfumo wa Android Oreo haujafikia watumiaji wa simu nyingi za Android. Google hufanya majaribio ya matoleo mapya kwa muda mrefu ili kuhakikisha mifumo hiyo inakuwa bora kwaajili ya watumiaji wa simu za Android.
Mwaka huu 2018, Google imeleta maboresho kadhaa kwenye mfumo huo mpya ikiwa pamoja na njia mpya ya kusoma maseji kupitia sehemu ya juu inayo onyesha ujumbe kabla ya kufungua pamoja na mambo mengine mengi.
Kwa sasa mfumo huo mpya wa majaribio wa Android P unaweza kupatikana kwa kuinstall kwenye simu za Pixel zinazo tengenezwa na kampuni ya Google. Ili kuinstall kwenye simu yako (kwa sasa aishauriwi) tembelea tovuti ya Google Android P hapa, kisha fuata maelekezo kwenye ukurasa huo.