Wote tunajua kuwa kwa hapa kwetu Tanzania watu wamekuwa waangalifu sana kuhusu MB zao, pengine hii ni kutokana na gharama za vifurushi hivi kuendelea kuongezeka kila siku.
Sasa kampuni ya Google imeliona hili na sasa inakuja na App mpya inayoitwa Datally, App hii itakusaidia kuwa na uwezo wa kutunza kiasi cha data au MB zinazotumiaka na programu mbalimbali kupitia simu yako.
Datally itaweza kukusaidia kujua ni programu gani inayotumia MB zako kwa wingi na ni kwa muda gani, vilevile app hii itakusaidia kuweza kuzuia app hiyo isiweze kutumia data mpaka pale utakapo amuwa wewe.
Kurahisha zaidi App hii itakuwa ikikuletea ujumbe maalum wa kuonyesha kuwa App fulani inatumia data kupita kiasi huku ikikuonyesha jinsi ya kudhibiti app hiyo isitumie MB zako kwa wingi. App ya Datally kwa sasa tayari inapatikana kupitia Play Store na unaweza kuipakua kwa kubofya hapo chini.
Nini maoni yako unaonaje App hii..? Je inakusaidia kutunza data zako kama Google inavyodai..? Jaribu App hiyo kisha tuambie kwenye maoni hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.