Kwa wale wasiojua project ara ni nini.. well project ara ni aina ya simu ambayo inatengenezwa na kampuni maarufu ya google, simu hii ambayo ni smartphone ina uwezo wa kutumia vifaa mbalimbali ambavyo unaweza kuvitoa na kuvirudisha vifaa hivi ni vile ambavyo kwenye simu za kawaida ni ngumu kuvitoa yani kama vile kioo cha simu yako, spika, kamera na vinginevyo.
Simu hii ilianza kutangazwa katikati ya mwaka jana ambapo ilisemekana kuwa simu hiyo ingetoka hivi karibu watengenezaji wa simu hiyo yani (Google) kupitia mkutano wake wa mwaka 2016 ujulikanao kama Google io ambao uliofanyika huko Amphitheater mountainview huko California ili tangaza kuwa sasa simu hiyo iko tayari kutoka, ikiwa imesha fanikiwa kutengeneza mfano wa simu hiyo Google ilitangaza kuwa simu hiyo itatoka rasmi mwanzoni mwa mwaka 2017 ambapo simu hiyo itakuwa tayari kuingia sokoni mwaka huohuo.
Kujua zaidi kuhusu Google Project Ara unaweza ukatembela website ya projectara.com au angalia video hiyo apo juu kujua zaidi.
Nimeipenda sana blog yenu endeleeni kutupa taarifa za teknolojia
Asante sana Mshindi Tupo pamoja sana