Baada ya Google kuamua kuachana na Majina ya Nexus pamoja na muundo mzima wa simu hiyo, sasa kampuni hiyo ya teknolojia ya nchini marekani inakuja na simu mpya iitwayo Google Pixel. Google Pixel ni simu ya kisasa ambayo inategemewa kutoka mwanzoni mwa mwezi October ikiwa ni simu yenye uwezo mkubwa kuliko simu nyingine ndani ya mwaka huu 2016.
Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali kutoka katika tovuti ya Android Police simu hiyo mpya ya Google Pixel inategemewa kutumia Processor mpya na ya kisasa ya Qualcomm’s Snapdragon 821, ikiwa ndio simu ya kwanza duniani kutumia processor ya aina hii.
Akielezea kwenye tovuti hiyo muandishi maarufu wa tovuti hiyo David Ruddock aliongezea akisema kuwa processor hizo za Qualcomm’s Snapdragon 821 zimetengenezwa ili kutoa uwezo wa asilimia 10% zaidi ya zile za Qualcomm’s Snapdragon 820 ambazo zinapatikana kwenye simu za Samsung Galaxy S7,S7 Edge, LG G5, HTC 10, Sony Xperia X Performance, Moto Z na Moto Z Force pamoja na nyingine nyingi ambazo zinafanya vizuri kwa sasa.
Simu hiyo ambayo inasemekana itapatikana kwa bei nafuu inawezekana ndio ikawa mkombozi wa soko la simu za Android baada ya simu mpya ya Samsung galaxy Note 7 kupatwa na janga la kulipuka kwa battery na kupelekea wasiwasi kwa watumiaji wa simu hizo kote duniani.
Kama unataka kujua ni tarehe ngapi Google watafanya uzinduzi wa simu hiyo ya Google Pixel ambayo inasemekana kwa sasa ndio itakua simu yenye nguvu kuliko zote duniani endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.