Kampuni maarufu ya Google ambayo ndio ina miliki mfumo wa Android leo imetangaza kuleta mfumo mpya wa Android O, mfumo huo mpya ambao sasa uko kwenye hatua za majaribio umekuja wakati toleo jipya la Android Nougat (Android N) likiwa hata bado halija sambaa sana kwa watumiaji wa Android duniani kote.
Mfumo huo wa Android kwa sasa umekuja na maboresho kadhaa ikiwemo uwezo wa simu inayotumia mfumo huo kukaa na chaji pamoja na maboresho mengine mbalimbali. Kuhusiana na Jina hilo la “Android O” bado haijajulikana jina kamili la mfumo huo kwa sababu mfumo huo bado uko kwenye hatua za majaribio kabla ya kuachiwa kwa watumiaji wote.
Vilevile mfumo huo utakuja na marekebisho ya kiusalama kwenye programu hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha jinsi mtumiaji wa mfumo huo anavyotumia proramu kutoka Play Store, ikiwa pamoja na kuongeza ubora wa kuongeza uwezo wa kuangalia video za youtube uku unatumia programu zingine kupitia mfumo huo mpya. Kwa sasa unaweza kudownload mfumo huo wa majaribio hapa lakini kumbuka mfumo huo hautakua umetulia hivyo ukiaribu simu yako hatuta husika pia kumbuka kuangalia kama simu yako inafaa kukubali mfumo huo.
Simu Zitakazo Kubali “Android O“ Mfumo wa Majaribio
- Nexus 5X
- Nexus 6P
- Nexus Player
- Pixel C
- Pixel
- Pixel XL
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa video.