Kampuni maarufu ya teknolojia ya Google hivi karibuni imetangaza kuacha kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe, kwa mujibu wa tovuti ya the information kampuni hiyo imeingia kwenye ushirikiano na kampuni ya Fiat Chrysler ambayo kwa kushirikiana na Google ndio itakayo toa matoleo ya gari hizo ifikapo mwaka 2017.
Hata hivyo kampuni ya Fiat Chrysler kwa sasa inamalizia kuitengenezea Google gari la kwanza linalojiendesha lenyewe lenye muundo wa Pacifica minivan ambalo kwa mujibu wa kampuni hiyo kama majaribio ya gari hilo yataenda kama inavyotakiwa, basi gari hilo litaingia sokoni moja kwa moja kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
Kwa muda kampuni ya Google imekua ikifanyia majaribio mbalimbali magari yake yanayojiendesha, ambayo baadhi ya majaribio hayo yamekua yakishindikana na magari hayo kuhusika kwenye ajali mbalimbali.
Google inategemea kutoa taarifa kamili ndani ya wiki hii, endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech tutakuhabarisha pindi Google watakapo tanganza rasmi habari hizi.