Habari mpya mihumu kwa watumiaji wa Android, hivi karibuni google itanza kufungia baadhi ya simu za android kutumia programu zake na hii ni kwa simu ambazo haziko Certified. Kwa mujibu wa tovuti ya theverge baadhi ya simu ambazo zitafungiwa ni pamoja na simu nyingi zinazotoka nchini china, yaani hizi ni zile ambazo zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kutumika nchini humo lakini unakuta unayo hapa Tanzania.
Kwa sasa Google watanza kuangalia tarehe ya uzalishaji inayokuwepo ndani ya mfumo wa undeshaji wa Android ambapo, kila mara unapotaka kupakua programu za Google tarehe hiyo maalum itaangaliwa ili kuruhusu programu hizo kupakuliwa kwenye simu yako. Sasa kuonyesha umuhimu wa jambo hili, binafsi nilipata meseji kutoka kampuni ya simu ya Airtel kunitaka kujua kuwa, Google watafungia baadhi ya simu kutumia programu zake hivyo niangalie na kuhakikisha simu yangu iko Certified.
Sasa ili kuhakiki simu yako ingia kwenye App ya Play Store kisha bofya sehemu ya juu upande wa kushoto alafu fungua ukurasa wa Settings, baada ya hapo sogea mpaka mwisho kabisa wa ukurasa huo kwenye sehemu ya Device certification utaweza kuona kama simu yako ipo Certified au Uncertified. Kama utakuta simu yako ipo Uncertified basi ni vyema ukajua kuwa simu yako itafungiwa kutumia programu za Google.
Unaweza ukawa unajiuliza programu za Google ni zipi..?, Sasa hapa programu za Google ni pamoja na programu kama Google Play Store, Gmail, Google, Google Map na nyingine kama hizo zilizo tengenezwa na kampuni ya Google. Muhimu hapa ni kuwa hutoweza tena kupakua programu kupitia Play Store sababu simu yako haitakuwa na uwezo wa kuingia au kutumia programu hiyo ya kutoka Google.
Sasa kuna wale ambao wanatumia Custom ROM kwenye simu zao za Android, kama wewe ni mmoja wa watu hawa angalau kuna habari njema kuhusu simu yako. Unachotakiwa kufanya ni kutuma Android ID ya simu yako kwa Google na google itafanya uhakiki wa ROM yako na kukuruhusu kutumia App za Google. Najua unajiluliza Android ID inapatikanaje.? kupata Androd ID install programu hiyo hapo chini, kisha fungua App hiyo alafu utaona Android Device ID kwa juu kisha ingia kwenye TOVUTI HII na weka Android Device ID yako hapo.
Kwa sasa Google bado haijasema ni sifa gani zinazofanya simu isemekane kuwa na Custom ROM kwa sababu hiyo basi, unaweza kujaribu njia hiyo hapo juu kwa simu yoyote ambayo ipo Uncertified pengine inaweza kufanya kazi kwenye simu yako. Tutawaletea muendelezo wa habari hii ikiwa pamoja na sifa za kujua simu yenye Custom ROM.