Google Kuongeza Maseji Maalumu Kwaajili ya Kuzuia Wizi wa Mitandaoni

Google Kuongeza Maseji Maalumu Kwaajili ya Kuzuia Wizi wa Mitandaoni Google Kuongeza Maseji Maalumu Kwaajili ya Kuzuia Wizi wa Mitandaoni

Mwezi uliopita kampuni ya Google ilileta mabadiliko mapya yaliyo tazamia katika kusaidia kuongeza ulizi katika kutuma pamoja na kupokea barua pepe yani Email, sehemu hiyo ya ulizi ilisaidia pale mtu anapotuma barua pepe kwenda kwenye barua pepe ambayo haiko salama. Sehemu hii ya ulizi imeonekana kusaidia sana kuongeza ulizi wa nyaraka za watu wanaotumia mitandao kote duniani.

Siku chache zilizo pita kampuni hiyo ilitangaza tena kuongeza viashiria maalumu mbavyo vitakua vikisaidia wateja wake kuperuzi mtandao kwa usalama zaidi, hata hivyo mwezi uliopita google iliweka vitambulisho hivyo kwaajili ya batani zisizo za kweli mitandaoni yani hizi ni zile unazokutana nazo zenye alama ya Play, nyingi ziko kwenye smartphone na hata kwenye baadhi ya website.

Advertisement

Hata hivyo kampuni hiyo imetangaza kuongeza ulinzi kwa kuongeza baadhi ya meseji kwa watumiaji wake pale wanapotaka kubonyeza link ambayo itapelekea wizi wa kimtandao. Meseji hizo zitasaidia kumpa mtumiaji wa mtandao taarifa maalumi itakayo mwambia kua link anayotaka kubonyeza sio salama, mfano wa meseji hiyo ni kama unavyoonekana kwenye picha hapo chini.

safe-browsing-gmail

Ili kuongeza ulizi kwenye email zako pamoja na usalama wa kuperuzi kwenye mtandaoni google itakuonyesha hatua kwa hatua namna ya kukusaidia pale utakapoona meseji hiyo kwenye screen yako.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use