Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Google Kulipa Dollar $100,000 kwa Yeyote Atakae Weza Ku-Hack Chromebook

Google Kulipa Dollar $100,000 kwa Yeyote Atakae Weza Ku-Hack Chromebook Google Kulipa Dollar $100,000 kwa Yeyote Atakae Weza Ku-Hack Chromebook

Google ni moja kati ya kampuni zinazojulikana duniani kwa kulipa Hackers yoyote duniani anaeweza ku-Hack mfumo wake wa ulinzi, hivi karibuni Google ilitangaza kumlipa hacker yoyote duniani anaweza ku-hack mfumo wake wa ulizi wa laptop yake mpya ijulikanayo kama Chromebook au Chromebox atakaye weza kufanya zoezi hilo atapewa dollar za kimarekani $100,000 sawa na zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 20.

Google ilitangaza ikisema mtu yoyote atakae weza kuhack mfumo wake wa ulizi kwenye laptop hiyo akiwa kama mtumiaji ambae hajasajiliwa kwenye laptop hiyo yani “Guest User” atalipwa kiasi hicho cha pesa, hii ikitegemewa kwamba Mfumo huo umetengeneza maalumu kwa kutenganisha mtumiaji mmiliki wa laptop hiyo na mtumiaji ambae anatumia laptop hiyo kwa mara ya kwanza.

Advertisement

Mwaka jana kampuni hiyo ya Google ilitangaza tena Kulipa kiasi cha Dollar za kimarekani million $2 kwa yoyote atakaye weza ku-hack mfumo wa ulinzi wa vifaa vya Chrome, lakini mpka sasa hajatokea mtu yeyote ambae amewahi kujinyakulia fungu hilo la bure kutoka kampuni ya Google yenye makao yake makuu huko marekani.

Kampuni hiyo iliendelea kutangaza kuwa hakuna kiasi cha mwisho cha kupata pesa hizo za bure yani, kama uliweza ku-hack mfumo huo kwa mara ya kwanza unaweza ukarudia tena mara ya pili na kila mara utakua ukijinyakulia kitita hicho cha dollar $100,000 bure kabisa.

Kama unataka kufanya zoezi hilo ilikujishindia zaidi ya shilingi milioni 20 bure kabisa Bofya Hapa usome vigezo na masharti ya kujiunga

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use