Google Kuifunga Application Yake ya Picasa

google-picasa google-picasa

Ijumaa moja Google walipost katika blog yao ya picasa ambayo haikuwahi kutumika kwa muda wa miaka minne, lengo la kupost katika blog yao hyo ni kuwapa taarifa watumiaji wa picasa kwamba application ya picasa na huduma zake zimefikia mwisho.

Hii ikiwa ni sababu Google wametengeneza application bora itakayo kuwa ikifanya kazi sawa na picasa, application hyo italenga zaidi watumiaji wa simu za mkononi maalumu kama smartphone. Moja ya sababu za kufungwa kwa application hiyo ni Google wanataka kuwa moja kati ya kampuni zinazo toa huduma za uhifadhi bora wa picha katika mtandao.

Advertisement

Hata hivyo kiongozi wa Google photo aitwaye Anil Sabharwal, amakaririwa akisema “baada ya kufikiria kwa kina tumefikiria kusitisha application ya picasa ndani ya mwezi ujao ili kuelekeza nguvu zetu kwenye application ya Google Photos”. Kiongozi huyo wa Google photo aliendelea kusema “tuna imani ya kuweza kutengeneza application moja bora zaidi ambayo italeta matumizi bora na marahisi katika simu pamoja na computer, kuliko kupoteza muda mwingi kushulikia application mbili tofauti” alisema Anil Sabharwal.

Hili sio jambo la kushanga kwa Google kufunga application hiyo ya picasa kuanzia ilipo anza kutumika mwaka 2004, kabla haijaanza kupungua watumiaji wake. Hii ikiwa na kutokana nakuanzishwa kwa application mpya ya Google Photo. Google inasibitisha kuwa application hiyo mpya ya Google Photo iliongezeka watumiaji zaidi ya milioni 100 mwezi October mwaka 2015. Hivyo kusababisha Google kuona haina budi kufunga application hiyo ya picasa, hata hivyo Google haija dhibitisha ni watu kiasi gani watakao adhirika na ufungwaji wa application hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use