Kampuni ya Google imejiandaa kuja na programu mpya ambayo inaitwa “Reply”, programu hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa watumiaji wa programu mbalimbali za kuchat kama WhatsApp, FB Messenger na nyingine kama hizo.
Programu hiyo mpya italeta sehemu maarufu ya “Reply” iliyo zoeleka kwenye programu ya kuchati ya Google Allo. Kama hujawahi kutumia programu hiyo ya Google Allo, sehemu ya Reply utokea kwenye kila meseji mpya unayo tumiwa na kutoa baadhi ya maoni juu ya jinsi ya kujibu meseji uliyo tumiwa bila kuandika.
Sasa kupitia programu hiyo mpya ya Reply, sehemu hiyo inakuja kwenye kila programu za kuchat kama WhatsApp, Facebook Messenger, Hangouts na programu nyingine kama hizo za ujumbe mfupi.
Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu programu hiyo mpya ya Reply kutoka Google inatumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence kuweza kutambua ni nini cha kujibu pale unapo tumiwa meseji kupitia mitandao mbalimbali.
Mitandao kamili ambayo inasemekana kuja kufanya kazi na programu hiyo ni mitandao ya Google Allo, Whatsapp, Facebook Messenger, Android Messages, Skype, Twitter DMs, pamoja na Slack. Kwa sasa programu hiyo bado haija tolewa lakini unaweza kujiunga ili kupata programu hiyo kwaajili ya majaribio kwa kujaza fomu hii HAPA kutoka Google.