Kama umekuwa unatumia huduma za Google kama vile YouTube, Play Store na huduma nyingine kama Gmail, Adsense na nyingine kama hizo basi lazima uliona kuto kupatikana kwa huduma hizo.
Hiyo ilitokana na Google kupata matatizo ya kiufundi kama ilivyo eleza kwenye ukurasa huu, kwa muda huo ulikuwa ukifungua email ya gmail inaonekana kama picha hapo chini.
TABLE OF CONTENTS
Updates Saa 04:24 EAT
Kwa sasa inaonekana tayari huduma za Google zimerejea kama kawaida na watumiaji wa huduma hizo kote duniani wameanza kuripoti kuendelea kutumia huduma hizo bila matatizo.
Hadi sasa Google bado haijatoa tamko rasmi nini chanzo cha huduma zake kuto kuwepo hewani kwa baadhi ya nchini, huku ikitoa taarifa kupitia Twitter kuwa inafahamu kuhusu Tatizo hilo.
Kilichotokea
Leo tarehe 14/12/2020, baadhi ya huduma za Google zilikosekana kwa muda kwa watumiaji mbalimbali kote duniani, huku huduma kama YouTube, Play Store na Gmail zikiwa zinaonekana kuto kupatikana kwa watumiaji wengi.
Hata hivyo tatizo hilo limeripotiwa kwa nchi mbalimbali kama vile ulaya, Marekani na nchi nyingine zilizo zinguka nchi hizo.
Kwa sasa tayari huduma hizo zimerudi hewani kama kawaida na bado Google haijatoa maelezo ya nini kilichotokea kusababisha kukosekana huko.