Roboti zinaonekana kuja kwa kasi sana kudhibitisha hilo hivi karibuni kampuni ya Piaggio yenye makao makuu yake huko Pontedera, Italy imezindua roboti mpya ya kukusaidia kubeba mizigo inayoitwa Gita.
Roboti hiyo ya Gita imetengenezwa kwa kutumia kamera maalum pamoja na mkanda ambao mtumiaji uvaa kiunoni na roboti hiyo ufuata mkanda huo uku ukiwa imebeba mizigo yako, roboti hiyo inatumia sehemu zote kama vile ilivyo pikipiki ndogo hivyo ina uwezo wa kutembea kwa kasi ya speed ya mile 22 kwa lisaa limoja ikiwa na uwezo wa kukufuata hata kama uko kwenye baskeli.
https://www.instagram.com/tv/CAxCZcSAaGc/
Vilevile Gita inauwezo wa wakutembea yenyewe baada ya kujua inapokwenda kwani roboti hiyo imetengenezwa na kuekewa ramani maalum ambayo hutumiwa na roboti hiyo baada ya kuionyesha njia kwa mara ya kwanza. Taarifa zote za mahali pa kwenda huifadhiwa kwenye ramani hiyo na baadae kutumiwa na roboti hiyo kujua unapotaka ipeleke mzigo wako.
Roboti hiyo ya Gita inategemewa kutoka mwezi huu na bado haijajulikana rasmi kuwa itauzwa kwa bei gani, watu wengi mtandaoni wanaonekana kupenda roboti hiyo na kusema kuwa itakuwa msaada mkubwa kwa watu wengi wanaotaka kubeba mizigo mingi wanapo kwenda mahali.