Inajuliakana duniani kua magari ya kisasa ni moja kati ya teknolojia kubwa sana hapa duniani, kuna magari yenye Touchscreen kama zile za smartphone na mengine yakitumia” advanced parking system” ambayo inatambua kama umepaki gari yako vibaya. Lakini hivi karibuni kampuni ya magari ya VOLVO imetangaza kutengeneza gari lake litumialo Application ya simu.
Kampuni hiyo ya magari ya nchini swedeni imepata wazo hilo la kutengeneza gari hilo litakalokua linatumia application ya simu yako kama funguo, ilikuwasha gari hilo unatakiwa kuwa na simu pamoja na application hiyo yenye password ambazo unaweza ku-share na ndugu na jamaa unaotaka waendeshe gari lako. Pia kama unataka kukodi gari kampuni ya ukodishaji magari inaweza kukutumia password hiyo itakayo kuwezesha kuendesha gari hiyo aina ya VOLVO.
VOLVO tayari inayo application maarufu ya kuangalia mafuta, kuangalia speed na ku-funga milango pia application hiyo inauwezo wa kutafuta gari yako popote ilipo kwa njia ya GPS pia application hiyo inauwezo wa kutoa msaada wa barabarani kama vile kuangalia barabara isiyo na foleni na vingine vingi.
Hata hivyo watengenezaji wa magari ya VOLVO walisema kwenye kipindi cha technology cha BBC kwamba utakapo poteza simu yako utakosa uwezo wa kuwasha gari yako, inakupasa kwenda kwa VOLVO “Dealership” ili kupata simu mpya na application mpya ili uweze kuwasha gari lako.