Kampuni ya Kitty Hawk ambayo inaendeshwa na kiongozi alie gundua mtandao wa Google Larry Page hivi karibuni imetangaza kuleta gari lake la kwanza linalo paa, Gari hili linauwezo wa kupaa baharini tu na kwa mujibu wa tovuti ya theverge ili kuendesha gari hilo haiku hitaji kuwa na leseni ya kuendesha ndege ili kuendesha gari hilo.
Gari hilo ambalo limepewa jina la Kitty Hawk Flyer linategemewa kutoka mwisho wa mwaka huu na kwa mujibu wa kampuni hiyo unaweza kujifunza kuendesha gari hilo kwa haraka sana. Gari hilo limepewa leseni na FAA na kuruhsiwa kuendeshwa bila leseni ya kuendesha ndege sababu ni jepesi sana hivyo hali itaji ujuzi wowote maalum.
Gari hilo linategemewa kuuzwa ndani ya marekani tu na bado hakuna ripoti zinazo sema kuhusu bei pamoja na siku maalum ambayo gari hilo litatoka. Kampuni hiyo ya Kitty Hawk inajulikana sana kwa uvumbuzi wake gari lingine linalo paa linalo julikana kama Zee Aero.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.