Ni wazi kuwa teknolojia inaendelea kukuwa sana hata hapa kwetu Tanzania, kudhirisha hayo kama una kumbuka hivi karibuni tumeona aina mpya ya teknolojia ya kuzuia wizi wa magari ambayo imebuniwa na vijana wa kitanzania, pia tumeona vijana wakitanzania wakibuni mifumo mingine mbalimbali ya kielektroniki.
Lakini kama hayo yote hayatoshi sasa kutana na kijana wa kitanzania aliyebuni gari la kwanza la kielektroniki hapa nchini Tanzania. Gari hili halina mfumo wa engine ya mafuta bali linatumia mfumo wa kielektroniki wa kuchaji.
Baada ya kuona ubunifu huu wa kitanzania nini maoni yako kuhusu gari hilo pamoja na teknolojia iliyotumika.? tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.