Hili Hapa ndio Gari la Gharama Kubwa Zaidi Duniani (2019)

Hadi sasa (2019) hili ndio gari la bei ghali zaidi duniani
Hili Hapa ndio Gari la Gharama Kubwa Zaidi Duniani (2019) Hili Hapa ndio Gari la Gharama Kubwa Zaidi Duniani (2019)

Kampuni ya kutengeneza magari ya nchini Ufaransa Bugatti, hapo siku ya jana imeonyesha gari lake jipya la bei ghali zaidi au la gharama kubwa kuliko yote duniani hadi sasa, Bugatti La Voiture Noir ndio gari la gharama kubwa hadi sasa mwaka 2019.

Gari hilo ambalo tayari limesha nunuliwa na mtu ambaye hakutajwa jina, linasemekana kuuzwa kwa dollar za marekani Milioni $11m ambayo ni sawa na takribani zaidi ya shilingi za Kitanzania Bilioni Tsh 25.7. Gari hilo ambalo limetengenezwa maalum kwa ajili ya kusherekea miaka 110 ya kampuni ya Bugatti, linasemekana kuwa la bei ghali zaidi kiasi cha kupita bei ya gari ambalo lilikuwa la gharama zaidi la Rolls-Royce Sweptail, lililo uzwa kwa kati ya Euro Milioni £8 – 9m Sawa na takribani Bilioni 24.7 za Kitanzania.

Advertisement

Gari hili kwa sasa bado halijulikani lina kasi gani, ila kwa mujibu wa tovuti ya BBC inasemekana Gari hilo limeonekana kuwa na sifa zinazo fanana na Bugatti Chiron, gari lingine kutoka kampuni hiyo lenye uwezo wa speed hadi kufikia mwendo wa 62mph kwa sekunde 2.4 na jumla ya speed ya 261mph.

Gari hili la Bugatti La Voiture Noire au kwa kiswahili Gari Jeusi, linasemekana kuja na engine yenye uwezo wa 1,500 horsepower pamoja na 16-cylinder engine, huku kama jina lake gari hilo limetengenezwa kwa rangi nyeusi huku pia siti zake zikiwa zimetengenezwa kwa kitambaa cha bei ghali zaidi.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, Gharama za gari hili zina ongezeka hadi kufikia dollar za marekani milioni $19 sawa na takribani Tsh Bilioni 44.9, Gharama hizo zikiwa zimechanganyiwa na gharama za kodi. Gari la Bugatti La Voiture Noire linawezekana kuingia kwenye list ya magari yenye kasi zaidi duniani, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha hayo kama gari hili lina speed ya kuweza kushindana na gari lenye speed kubwa kwa sasa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use