Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kudownload Game za Kompyuta (EPIC Games) Bure

Utaweza kudownload game kama Fortinite, GTA V, Unreal Tournament na nyingine bure 100%
Jinsi ya Kudownload Game za Kompyuta (EPIC Games) Bure Jinsi ya Kudownload Game za Kompyuta (EPIC Games) Bure

Kama wewe ni mpenzi wa game za kompyuta basi najua unatumiaga muda mwingi sana kutafuta games za bure za kucheza kwenye kompyuta yako. Lakini kuanzia sasa huna haja ya kuendelea kuangaika tena kwani kupitia makala hii nitakuonyesha jinsi rahisi ya kudownload games za kompyuta za Epic Games bure kabisa.

Njia hii ni rahisi na ni maalum kwa watumiaji wa kompyuta, kumbuka unatakiwa kudownload game hizi kwenye kompyuta yako hivyo hakikisha unalo bando la kutosha kabla ya kuendelea. Games hizi kuna wakati zinakuja na hadi GB 22 na kuendelea, hivyo ni vizuri kuangalia bando la bei rahisi.

Advertisement

Sasa baada ya kusema hayo moja kwa moja ngoja nikwambie njia ya kupata game hizi za kompyuta bure kabisa bila kulipia. Njia hii ni halali kwa aslimia 100 na utapata game ambayo unaweza ku-update au kusasisha kila itakapo ongezewa kwenye kifaa chako.

Unchotakiwa kufanya ni kutengeneza akaunti ya Epic Games kupitia link hapo chini. Ambapo kupitia tovuti hiyo wanatoa game za bure kila wiki siku ya jumatano. Utaweza kupakua game hiyo kwenye kifaa chako na utaweza kutumia kadri utakavyo.

Tengeneza Akaunti Bure Hapa

Jinsi ya Kudownload Game za Kompyuta (EPIC Games) Bure

Baada ya kutengeneza akaunti, unaweza kurudi kwenye tovuti hii na bofya link hapo chini na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kupakua Games mbalimbali za kompyuta kutoka Epic Games bure kabisa bila kulipia. Bofya Hapo chini Kujiunga au kama unayo akaunti utapelekwa kwenye ukurasa wa kupakua game moja kwa moja kwenye kompyuta yako.

Download Game za Bure Hapa

Pia kupitia link hii unaweza kuwa unapata games mbalimbali za bure kabisa kupitia kwenye store ya Epic Games, hivyo kama umekosa game hii ya uliyokuwa unataka unaweza kutumia link hiyo kupata games nyingine za premium edition kwa kuhakikisha una tembelea link hii kila wiki.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use