Wakati ikiwa bado China na Merakani zikiwa kwenye migogoro ya kibiashara, nchini India pia hali ya uhusiano wa China na India inaendelea kuharibika.
Baada ya serikali ya India kuzuia apps mbalimbali zaidi ya 58 za China kutumika nchini India, hatimaye hivi leo serikali ya India imetangaza kuzuia app nyingine 117 za China ikiwepo game maarufu ya PUBG.
Government blocks 118 mobile apps which are prejudicial to sovereignty and integrity of India, Defence of India, Security of State and Public Order: Govt of India
PUBG MOBILE Nordic Map: Livik, PUBG MOBILE LITE, WeChat Work & WeChat reading are among the banned mobile apps. pic.twitter.com/VWrg3WUnO8
— ANI (@ANI) September 2, 2020
Hadi sasa bado serikali ya india imesema sababu ya kuzuia apps hizo ni kutokuwa salama kwa matumizi ya wananchi wake. Hadi sasa India inakuwa imezifungia jumla ya apps 167 kutoka nchini China.
Kwenye list hiyo, app nyingine maarufu ukitoa game ya PUBG ni pamoja na Rise of Kingdoms, Art of Conquest, Arena of Valor na nyingine. Kwa mujibu wa tovuti ya Beebom, hadi sasa bado game hizi na baadhi ya app zinafanyakazi kwenye simu za watu waliokuwa wamepakua app hizo nchini India, lakini pengine hiyo inaweza isiendelee kuwa hivyo kwa muda mrefu.