Kampuni ya teknolojia pamoja na utengenezaji wa Video Game ya Ubisoft, hivi karibuni imesherekea miaka 30 toka kuanzishwa kwa kampuni hiyo ambayo sasa ni moja kati ya kampuni kubwa sana zinazojihusisha na utengenezaji wa Video Game.
Katika kusherekea miaka hiyo kampuni hiyo ilianza kutoa game zake maalum bure kabisa, game ya Assassin’s Creed III ni game ya 15 kwenye mtiririko wa game za bure ambazo kampuni hiyo ilipanga kuzitoa bure kabisa kwa watumiaji wake.
Game hiyo ya ni moja kati ya game nzuri sana kwa wapenda game wote duniani kwani imeshirikisha stori nzuri pamoja na Action kwa wale wanaopenda game za namna hiyo, vilevile Assassin’s Creed ni moja kati ya game zile ambazo zimekubalika sana kiasi cha kutengenezewa filamu yake, ili kujua kidogo kuhusu game hii angalia trailer ya game hiyo hapo chini.
Ili kudownload game hiyo utatakiwa kujiunga na kutengeneza akaunti kwenye tovuti ya ubisoft na hapo utaweza kudownload game hiyo yenye GB 16 bure kabisa. Kama unataka kudownload game hiyo kabla ofa hiyo haija isha bofya Hapa.
Filamu ya game hii inategemewa kutoka hapo kesho tarehe 12 mwaka 2016 na kwa kuangalia tu trailer ya filamu hii inaonekana ni moja kati ya filamu ambazo zitakua bora sana za kufungia mwaka huu 2016.
Kwa habari zaidi za (game) michezo unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.
Maoni* Kiukwel Hizo Simu Ni Nzur Nimezipenda Hata Mimi Tunaomb Mtuletee Hadi Kijijini