Watu wengi sana hupenda kucheza game kwenye simu zao, mara nyingi hii imekuwa ni utaratibu wa watu wengi kutokana na game hizi kuwa nzuri sana na kwa watu wengine hii imekuwa kama ni dawa ya kupunguza msongo wa mawazo.
Sasa kama umekuwa ni mpenzi wa kucheza game kwenye simu yako kwa namna yoyote, leo Tanzania Tech tunakuletea Game nzuri za Android pamoja na iOS ambazo na uhakika kwa namna moja ama nyingine utafurahia game hizo. Basi baada ya kusema yote hayo sasa twende tukaangalie game hizi.
1. Knife Hit
- Android
- iOS
Kama bado hujawahi kucheza Game hii ya Knife Hit basi nakwambia unapitwa sana. Game hii itakupa uwezo wa kurusha visu kwenye mbao mpaka utakapo maliza kuivunja. Game hii ni nzuri sana na ukweli nakushauri jaribu tu alafu uniambie kwenye maoni hapo chini.
2. Rally Racer Evo – Android
Game nyingine ambayo ni nzuri sana kujaribu ni Rally Racer Evo. Game hii ni nzuri sana na inakupa uwezo wa kuendesha magari mbalimbali ambayo ili kuyapata lazima uweze kupata leseni, Game hii ni nzuri sana na ukweli ukijaribu utaipenda sana. Kwa sasa game hii bado haipo kwenye mfumo wa iOS.
2. Into The Dead 2
- Android
- iOS
Game nyingine nzuri ni game ya Into The Dead 2, Game hii ni nzuri sana na itakupa uwezo wa kufurahia simu yako. Ndani ya game hii utaweza kuuwa ma-zombie na utaweza kutumia silaha mbalimbali ambazo utaweza kuzipata kadri unavyo endelea kucheza game hii.
3. Big Hunter
- Android
- iOS
Kama kwa namna yoyote umefurahia game ya kwanza kwenye list hii basi utaweza kufurahia game hii pia. Ndani ya game hii itakuwa na uwezo wa kuwinda wanyama na kuwauwa kwa kutumia mishale. Game hii ni nzuri sana guys na mpaka sasa mimi mwenyewe nacheza game hii, kama unasimu ya android au ios basi nakushauri jaribu game hii sasa.
4. Skateboard Party 3
- Android
- iOS
Kama kwa namna yoyote wewe ni mpenzi wa Skateboard basi Skateboard Party 3 ni game nzuri sana kwako. Ndani ya game hii utaweza kuendesha Skateboard na utashindana na watu mbalimbali duniani na pia utaweza kucheza mwenye kama utakuwa unapenda.
5. WGT Golf
- Android
- iOS
Kama ulisha wahi kucheza mchezo wa Golf au kama unataka kujifunza basi game hii ya WGT Golf ni game nzuri sana kwako, Game hii ni nzuri sana na inamuonekano mzuri sana na nakuhakikishia utafurahia kuicheza. Ijaribu sasa kisha niambie maoni yako hapo chini.
Na hizo ndio game nzuri za android na iOS nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama wewe ni mpenzi wa game za mpira unaweza kusoma makala yetu iliyopita, pia kama unataka game zaidi unaweza kusoma makala yetu nyingine hapa na uhakikia utapata game nyingine nzuri za kucheza kwenye simu yako.
Kwa habari na maujanja mbalimbali ya Teknolojia hakikisha unapakuwa app yetu ya Tanzania Tech kwa Android pamoja na iOS.
Daaah sikuwahi kujutia kuwajuua nyie maana kila siku mnanipa elim mpya kila siku
Asante sana, Endelea kutembelea Tanzania Tech.