Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Game Nzuri za Kucheza Kwenye Simu ya Android

Furahia Weekend Yako kwa kucheza Game hizi kwenye simu yako ya Android
Game za Android Game za Android

Muda mwingi wakati akili zetu zimechoka kutokana na shughuli za siku nzima tunapenda kutumia muda huo kuweza kupumzika huku tukifanya mambo mbalimbali kupitia simu zetu za mkononi.

Kuliona hilo siku ya leo nimekuletea list hii ya game nzuri za Android ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako ya Android ambazo naimani zinaweza kukusaidia kupumzika vizuri na kukufanya ufurahie zaidi muda wako wa mapumziko. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii.

Advertisement

Kama wewe ni mpenzi wa Game basi lazima utakuwa unaijua Game ya PUBG, Game hii ni moja kati ya Game nzuri sana za kucheza kwenye simu yako ya Android kwani zinamuonekano mzuri sana na ukweli utafurahia kucheza game hii.

Download Hapa

MARVEL Strike Force ni Game nyingie nzuri ambapo unatakiwa kupambana na aina mbalimbali za maadui ambao wamekuja kuangamiza dunia Game hii ni nzuri kwa sababu imechanganya Super Heros mbalimbali kutoka kwenye filamu mbalimbali unaweza kuipakua sasa na ujionee mwenyewe.

Download Hapa

Shadow Fight 3 ni mfululizo wa Game nzuri sana ambapo unapambana na vivuli mbalimbali vya watu baada ya ulimwengu kukubwa na giza baada ya kuachiwa kwa aina fulani ya laana. Game hii ni nzuri sana na kama wewe unapendelea Game za kupigana basi hii ni game nzuri sana ya kujaribu.

Download Hapa

Hii ni Game nyingine nzuri sana kwa wapenzi wa Game, Game hii inakuruhusu kupambana na viumbe mbalimbali kutoka nje ya dunia na unafanya vyote hivyo kwa kutumia nguo na silaa maalum, unaweza kuchagua aina mbalimbali za nguo pamoja na silaha.

Download Hapa

Kwa wale wapenzi wa PS kutoka miaka ya zamani lazima utakuwa unafahamu game hii ya call of duty, Game hii inakuruhusu kuweza kupigana na vikosi vya watu mbalimbali ili kuweza kuchukua point zaidi pamoja na kukutana na wachezaji wakubwa zaidi. Kama wewe ni mpenzi wa Game za kupigana hakikisha unapakua Game hii.

Download Hapa

Kama ulisha wahi kutazama Tamthilia ya The Walking Dead na ukaipenda basi ni lazima utaipenda game hii pia, Game hii inakupa uwezo wa kupambana na Mazombi… mbalimbali kwa kutumia sila mbalimbali ambazo unaweza kuzipata kadri unavyozidi kucheza game hii.

Download Hapa

Bullet Force ni Game nyingine ya Android ambayo ni nzuri kucheza, Game hii inakupa uwezo wa kutumia silaha mbalimbali kwa kupambana kivita na wachezaji wengine na utakuwa na uwezo wa kucheza pamoja na marafiki zako moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.

Download Hapa

Kama wewe ni mpenzi wa Game za pikipiki basi game hii ni Game nzuri sana kucheza. Game hii ni nzuri sana na unaweza kucheza bila hata kuwa na internet kwenye simu yako, Kingine kizuri kuhusu game hii ni kuhusu ukubwa wake, game hii ni ndogo kwa ukubwa kuliko game nyingine kwenye list hii.

Download Hapa

Kwa wale wapenzi wa Game za Mpira wa kikapu basi ni vyema ukajaribu game hii, Game hii ni nzuri sana na ukuweli mbali ya muonekano wake Game hii ni bora sana hasa kwa wale wanao elewa na kupenda mpira wa kikapu. Utaweza kuunda timu yako pamoja na kushindana kwenye mashindano mbalimbali na timu nyingine.

Download Hapa

Sina haja ya kusema sana kuhusu Game hii na kama kweli bado hujafanikiwa kucheza game hii basi ni wakati sasa wa kujaribu game hii. Unaweza kushindana na watu mbalimbali duniani kwa kupigana nao kupitia game hili pia unaweza kuongeza uwezo wa wapiganaji wako kadri unavyo cheza mara kwa mara.

Download Hapa

Na hizo ndio game nilizo kuandali kwa siku ya leo unaweza kusoma programu nyingine za android ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako kwa kupitia makala iliyopita. Mpaka wiki ijayo nakutakia weekend njema.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use