Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tetesi Samsung Galaxy S8 Kuja na Kioo Kitupu kwa Mbele

Tetesi hivi karibuni samsung galaxy s8 inategemewa kuja na kioo kitupu kwa mbele bila kava la plastic juu na chini
Samsung Galaxy s8 Samsung Galaxy s8

Tetesi zinaendelea kuvuma sana kuhusu simu mpya ya Samsung Galaxy S8, na leo zimezuka tena tetesi zingine kuhusu simu hiyo zikiwa zinasema kuwa huenda simu hiyo mpya ya Galaxy s 8 ikaja bila kuwa na makava ya plastic kwa juu na chini yaani simu hiyo itakua ni kioo kitupu kwa mbele.

Tetesi hizi zimesambaa leo kutoka kwenye tovuti ya Bloomberg zikiwa zinaendana na tetesi za kwenye tovuti ya The next web, ambazo zilikua zinadai kuwa simu hiyo haitakuwa na kitufe cha Home ili kuwezesha simu hiyo kuwa kuwa na kioo kitupu.

Advertisement

Kwasasa tetesi za simu hiyo ya Samsung Galaxy S8 zimekua nyingi sana, tumesha sikia tetesi za simu hiyo kuja na kioo cha 4K na baadae tetesi hizo zilikanushwa kwa kusemekana ni kioo cha 2k pamoja na tetesi nyingine nyingi za kuhusu simu hiyo ya Samsung Galaxy S8 inayotegemewa kutoka mwezi February 2017 huko Barcelona kwenye mkutano wa Mobile World Congress.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use