Ni miezi michache imebakia mpaka kuzinduliwa rasmi kwa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9, na kama tunavyojua kadri siku zinapozidi kukaribia tetesi nazo zina endelea kufurika kwa kasi zaidi, moja kati ya tetesi ambayo nimeona leo nikusogezee ni hii ya Galaxy Note 9 kuja na ukubwa wa ndani wa GB 512.
Kwa mujibu wa tetesi kutoka kwa mvujishaji maarufu kwenye mtandao wa Twitter anaeitwa Ice Universe, Samsung Galaxy Note 9 inategemewa kuja na toleo jipya lenye ukubwa wa Ndani wa GB 512, kwa mujibu wa tetesi hizo simu mpya ya Galaxy Note 9 itakuwa ndio simu ya kwanza kutoka kampuni ya Samsung yenye uwezo huo wa ukubwa wa ndani na pia ndio simu ya kwanza kutoka samsung yenye uwezo wa RAM ya GB 8.
Mbali na tetesi hizo, tetesi nyingine zinadai kuwa, Galaxy Note 9 itakuwa pia ndio simu ya kwanza kutoka kampuni ya Samsung kuja ikiwa na teknolojia mpya ya Fingerprint juu ya kioo.
Siku za nyuma kidogo tuliona simu ya kwanza yenye ukubwa wa ndani wa GB 1000 na baadae tukasikia habari nyingine kuhusu ujio wa simu mpya ya Lenovo Z5 ambayo yenyewe inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 4000. Kuwepo kwa simu hizo kuna onyesha inawezekana kabisa tetesi za Galaxy Note 9 kuja na ukubwa wa ndani wa GB 512 zikawa zina ukweli ndani yake, Mara nyingi kampuni ya Samsung imekuwa ikipenda kushindana hasa kwenye maswala mengi yanayohusu ubunifu wa teknolojia za simu za mkononi, hivyo ni wazi samsung itafanya jitihada za kushindana na hao walio tangulia kwa kuja na simu yake yenye ukubwa huo wa ndani wa GB 512
Vipi kwa upande wako unaonaje..? Je unadhani kuna uwezekano wa Samsung kuja na simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 512 mwaka huu..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.