Kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung basi ni wazi unajua kuwa kampuni ya Samsung inajiandaa kuja na simu mpya ya Galaxy Note 10. Simu hii ni toleo la maboresho la simu ya Galaxy Note 9 ambayo ilizinduliwa mwezi August mwaka jana 2018.
Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, inasemekana kuwa simu hiyo mpya ya Galaxy Note 10 inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 7 mwezi wa nane mwaka huu 2019. Kama ulikuwa hujui, wiki hii kumekuwa na tetesi mbalimbali ambapo picha mbalimbali zimesha vuja mtandao zikionyesha muonekano unao semekana ndio muonekano halisi wa simu hiyo mpya.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, muonekano wa simu hizo ndio unaosemekana kuwa muonekano halisi wa Galaxy Note 10. Hata hivyo taarifa hizo za tetesi zinasema kuwa, mwaka huu Galaxy Note 10 inatakuja na matoleo mawili huku toleo jipya likiwa limepewa jina la Galaxy Note 10 Pro.
Kwenye picha hapo juu, Galaxy Note 10 Pro ipo upande wa kushoto na Galaxy Note 10 ipo upande wa kulia. Vilevile inasemekana kuwa simu hizo mbili zitakuwa na muonekano unao fanana lakini utofauti mkubwa utakuwa ni kioo kikubwa pamoja na kamera za ziada kwa nyuma kwenye simu mpya ya Galaxy Note 10 Pro.
Mbali na hayo tetesi hizo kutoka tovuti ya 91mobiles, zimeongeza kuwa, Galaxy Note 10 itakuja ikiwa inaendeshwa na processor yenye nguvu ya Snapdragon 855 ambayo itakuwa inasaidiwa na RAM ya GB 12 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 512, hata hivyo ukubwa huo utakuwa unaweza kuongezewa na memory card ya hadi Terabyte 1.
Kwa sasa hayo ndio machache kuhusu simu mpya ya Galaxy Note 10, kama unataka kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku au subscribe kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube.
Ningependa utujuze kuhusu ubora wa processor wa simu kama hizi mediatek na snapdragon