Samsung Galaxy C5 Pro ya mwaka (2017) ni moja kati ya simu za daraja la kati kutoka kampuni ya Samsung. Simu hii imetengenezwa maalum kwaajili ya soko la nchini China lakini hadi kufikia mwaka jana samsung imeanza kuuza simu hizi nje ya soko la nchini China.
Kwa upande wa sifa za simu hii samsung imefanya kazi nzuri sana kupitia simu hizi kwani simu hii ina sifa nzuri sana ambazo zinaweza kushindana na baadhi ya simu za daraja la kwanza kama vile Galaxy S8, na nyingine kama hizo.
Kwa ufupi kabisa Galaxy C5 Pro inakuja na processor ya Qualcomm MSM8953-Pro Snapdragon 626, RAM ya GB 4, ukubwa wa ndani hadi GB 64 ambao unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 256. Kamera ya mbele ya simu hii inakuja na uwezo wa Megapixel 16 na nyuma pia inakuja na uwezo wa Megapixel 16.
Kwa upande wa mfumo simu hii inatumia mfumo wa Android Nougat 7.0, mfumo ambapo sasa Samsung imeanza kufanya majaribio ya mfumo mpya wa Android 8.0 ambao unategemewa kupatikana rasmi kwenye simu hii baadae mwaka huu. Hata hivyo kwa watumiaji wa simu za Galaxy C7, C7 Pro, C9 na C9 Pro ripoti kutoka tovuti ya The Android Soul zinasema kuwa, simu hizo pia zinategemewa kupata toleo hilo jipya la Android 8.0 Oreo baadae mwaka huu.
Simu za toleo la Galaxy C ni moja kati ya simu bora za daraja la kati kutoka kampuni ya Samsung, simu hizi zinapendwa zaidi na watu mbalimbali duniani kote kutokana na uwezo wake mkubwa unaoweza kushindanishwa na simu zenye majina makubwa zaidi kwa sasa. Kwa hapa Tanzania unaweza kupata simu hizi kwa bei ya makadirio kuanzia Tsh 800,000 hadi Tsh 600,000 kupitia maduka mbalimbali, kumbuka bei hiyo inaweza kubadilika.