Galaxy A70 ni simu mpya ya Samsung ambayo imeingia sokoni takribani mwezi mmoja na nusu hivi, lakini kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya etnews ya korea, inasemekana Samsung inajiandaa kuja na toleo lingine la simu hiyo ambayo itakuwa inaitwa Galaxy A70s.
Mbali ya toleo hili kuwa ni toleo la maboresho la simu mpya ya Galaxy A70, simu hii pia itakuwa ni simu ya kwanza kutoka kampuni ya Samsung kuwa na kamera yenye uwezo wa hadi Megapixel 64. Kampuni ya Samsung itakuwa ni moja kati ya kampuni za kwanza kabisa kutoa simu zenye uwezo huu wa kamera, uwezo ambao unasemekana ndio mkubwa zaidi kwenye simu za mkononi.
Kwa sasa zipo simu nyingi tofauti zenye kamera ya Megapixel 48, hivyo sio ajabu kuona simu kama Galaxy A70s zenye kamera ya Megapixel 64 kuanza kuzinduliwa zaidi mwishoni au mwanzoni mwa mwaka ujao 2020.
Kama unakumbuka, Mkurugenzi mtendaji wa usaidizi wa bidhaa wa kampuni maarufu ya kutengeneza processor ya Qualcomm, alisema kuwa kwa mwaka huu tutegemee kuona simu zenye uwezo wa kamera wa hadi Megapixel 64 na 100. Hata hivyo sababu za mkurugenzi huyo kusema hivyo ni pamoja na ujio wa processor mpya kutoka Qualcomm za Snapdragon 865, processor ambazo zinasemekana kuwa na nguvu kubwa ya kuendesha kamera zenye uwezo huo.
Hata hivyo, Galaxy A70s inasemekana kuzinduliwa kati ya nusu ya pili ya mwaka 2019, ambapo simu hiyo inategemea kuja na teknolojia ya Tetracell technology kwenye kamera yake, teknolojia ambayo inafanya kamera ya simu hiyo kuchukua picha nzuri zaidi na kuongeza mwanga kwenye picha ambazo zinapigwa kwenye mwanga mdogo.
Kwa habari zaidi kuhusu simu hii pindi itakapo toka endelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech, pia hakikisha una subscribe kwenye channel yetu kuweza kuona muonekano wa simu hii pindi itakapo toka rasmi.
Iko vizur sn Nokia A70s