Samsung Galaxy A10 na Galaxy A20e Zapata Android 10

Unatumia simu za Galaxy A10 na Galaxy A20e sasa unaweza kupata Android 10
Samsung Galaxy A10 na Galaxy A20e Zapata Android 10 Samsung Galaxy A10 na Galaxy A20e Zapata Android 10

Kampuni ya Samsung ni moja kati ya kampuni ambazo zinaongoza kwa ku-update au kusasisha matoleo mapya ya Android kwenye simu zake. Hivi karibuni kampuni hiyo imetangaza kutoa mfumo mpya wa Android 10 kwa ajili ya simu za za daraja la kati za Samsung Galaxy A10 pamoja na Galaxy A20e.

Samsung Galaxy A10 na Galaxy A20e Zapata Android 10

Advertisement

Kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanatumia simu hizi basi hakikisha una angalia update kwenye simu yako kwani toleo hili jipya la Android 10 tayari linapatikana moja kwa moja. Ili kuangalia update ingia kwenye simu yako bofya sehemu ya Settings > Software update > Download update manually. Baada ya hapo utaweza kuona update zitafuta na utaweza kupakua mfumo mpya wa Android 10 kwenye simu yako.

Samsung Galaxy A10 na Galaxy A20e Zapata Android 10

Mfumo wa Android 10 unakuja na mabadiliko mengi sana, mabadiliko ambayo vile vile yanakuja na mfumo mpya wa Samsung One UI 2 mfumo ambao unakuja na maboresho mapya pamoja na muonekano wa kisasa.

Kwa sasa bado Samsung inaendelea ku-update simu zake kwenda kwenye mfumo wa Android 10 huku bado zikiwa simu nyingine nyingi zikiwa zikisubiri kupokea mfumo huo. Unaweza kusoma hapa kujua kama simu yako ipo kwenye list ya simu zitakazo pokea mfumo wa Android 10. Bado mpaka sasa tunaendelea kusubiri update za Android 10 kwa simu za TECNO kama ilivyo ahidiwa mwaka jana na kampuni hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use