Jinsi ya Kuwezesha FM Radio Kwenye Simu Yoyote ya Android

Hatua za Kuwezesha FM Radio kwenye simu yoyote ya Android
FM Radio kwenye Android FM Radio kwenye Android

Baadhi ya watu hapa Tanzania na baadhi ya nchi, simu kuwa na FM Radio ni kitu cha msingi sana kwani inakusaidia kupata matangazo mbalimbali ya Radio moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi. Lakini kunawakati unanunua simu nzuri sana na umeipenda kwa asilimia 100 lakini ghafla unakuta haika kitu kimoja cha muhimu sana ambacho ni FM Radio.

Sasa hapa Tanzania Tech tumepata suluhisho la swala hili na sasa unaweza kuwezesha sehemu ya Radio kwenye simu yako moja kwa moja. Sehemu hii haitumii Internet na inakuwa inafanya kazi kama Radio ya kawaida ya kwenye simu za mkononi. Unachotakiwa kufanya ni kuchomeka Headphone au Earphone kwaajili ya kuwezesha antena na radio itaweza kufanya kazi.

Advertisement

Lakini kabla ya kuanza labda nifafanue kidogo kuhusu maujanja haya. Kwanza ili kusudi simu yako iweze kufanya kazi kupitia maujanja haya ni lazima simu yako iwe inayo sakiti yenye kifaa kinachowezesha FM Radio. Mara nyingi kampuni nyingi zinazo tengeneza simu, zinaweza kutumia kifaa hicho ndani ya simu husika lakini kusiwepo na Radio kwenye simu hiyo, badala yake kifaa hicho hutumika kwa kazi zingine za ziada.

Sasa kwa kutumia njia hii utaweza kuwezesha matumizi ya kifaa hicho na utaweza kuweka sehemu ya Radio moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi (Smartphone). Sasa baada ya kusema yote hayo sasa twende kwenye maujanja yenyewe.

Njia ya Kwanza #1 ( Next Radio )

Kwenye njia hii tutaenda kutumia programu ya Android ya Next Radio, programu hii inawezesha kusikiliza radio zote za internet pamoja na Radio za kawaida za FM ambazo hazitumii Internet.

  • Hatua ya Kwanza (Angalia Kama Simu Yako Inauwezo wa Radio)

Hatua ya kwanza unachotakiwa kufanya ni kuangalia kama simu yako inao uwezo wa kuwezesha FM Radio kwa kutumia maujanja haya. Kufanya hivyo tembelea tovuti hii, kisha angalia kama jina la simu yako lipo kwenye list ya majina ya simu zilizo ainishwa hapo kwenye ukurasa huo. Kurahisha kazi kama wewe unatumia Galaxy S9 au S9 Plus, au Galaxy S8, Galaxy S7 basi unaweza kuendelea na hatua inayofuata kwani simu hizi zinauwezo wa kutumia njia hii moja kwa moja.

  • Hatua ya Pili (Pakua App ya Kuwezesha FM Radio)

Kama tayari umeona simu yako au kama ujaona simu yako na unataka kujaribu njia hii basi hatua inayofuata ni kupakua app ya Next Radio, App hii ndio yenye uwezo wa kuwezesha radio na inafanya hivyo kwa kutumia vifaa ambavyo tayari viko ndani ya simu yako ili kuwezesha sehemu hiyo. App hii inapatikana Play Store ila kwa baadhi ya watu unaweza usiweze kupakua app hiyo kupitia Play Store. Kama ikitokea umeshindwa kupakua app hiyo unaweza kuipakua kupitia link HAPA. Kama unataka kujaribu kupakua kupitia Play Store basi tumia link hapo chini.

  • NextRadio Free Live FM Radio
  • Hatua ya Tatu (Washa FM Radio Isiyo Tumia Internet) 

Jambo la muhimu ni kujua application hii inakuja na sehemu mbili muhimu, inakuja na sehemu ya kusikilza Radio za Internet na sehemu ya kusikiliza Radio bila Internet. Sasa ili kuwasha sehemu ya kusikiliza Radio bila internet bofya Setting kwenye app hiyo, kisha bofya Interface kisha bofya Switch to Tuner Mode. Baada ya hapo unatakiwa ujue frequency za radio unayotaka kusikiliza kwa mfano kama unataka kusikiliza Clouds FM na uko Dar es salaam basi unaweza kutumia Frequency za 88.5, baada ya hapo utaweza kusikiliza Radio bila kutumia Internet moja kwa moja.

Njia ya Pili #2 ( Spirit FM )

Kama kwa namna yoyote njia ya kwanza imeshindikana basi ni wakati wa kujaribu njia hii ya pili. Kwenye njia hii ya pili tunatumia programu ya Spirit FM, Programu hii inahitaji uwe umeroot simu yako kama simu yao haijawa rooted basi ni vyema kutumia njia ya kwanza au kama unataka kujifunza kuroot simu yako basi unaweza kusoma hapa, baada ya hapo endelea kwa kufuata hatua hapo chini.

  • Hatua ya Kwanza (Pakua App ya Spirit FM)

Kwa sasa app ya Spirit FM Haipatikani kwenye masoko ya Play Store hivyo inakubidi kupakua App hii kupitia link HAPA, baada ya hapo hakikisha simu yako iko rooted kisha washa programu hiyo.

  • Hatua ya Pili (Washa App Hiyo na Weka Frequency)

Baada ya hapo sasa washa app hii, na kama simu yako tayari iko rooted basi hakikisha app ya Spirit FM inaruhusu kutumia SuperSU, baada ya hapo endelea kwa kuweka headphone kwenye simu yako kisha washa FM Radio kwenye kitufe cha kuwasha cha Rangi nyekundu kisha weka Frequency za Radio unayotaka kusikiliza.

Kama utakuwa umefuata hatua zote hizi na uhakika kwa namna moja ama nyingine utakuwa umewezesha sehemu ya FM Radio kwenye simu yako ya Android. Kama njia zote zimekataa tuambie kwenye maoni hapo chini tutajitahidi kukusaidia, Pia kwa maujanja zaidi unaweza kujiunga nasi kupitia Telegram hapa Tanzania Tech.

9 comments
  1. Mbali na redio za fm kuwa kwenye simu nyingi, nauliza na hizi redio za masafa ya kati zinaweza kupatikana kwenye simu janja?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use