Ni wazi kuwa teknolojia inakuwa kila siku, Miaka ya karibuni tulisikia USB flash drive yenye TB 1 ndio flash kubwa zaidi, miezi michache baadae tukasikia Flash ya TB 2 ndio flash kubwa kuliko zote duniani. Lakini kama haitoshi sasa mwaka 2019 kuna USB flash nyingine ambayo sasa ndio kubwa zaidi duniani yenye ukubwa wa TB 4.
Kupitia mkutano wa CES 2019 kampuni ya Western Digital imezindua USB flash Drive ya SanDisk ambayo inakuja na uwezo wa TB 4 kuhu ikiwa ndio flash Drive iliyoshikilia taji la kuwa flash yenye ukubwa mkubwa zaidi Duniani.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali inasemekana kuwa Flash Drive hiyo inakuja na speed kubwa na unaweza kuhifadhi vitu mbalimbali bila kuwa na wasiwasi wa speed yake wakati wa ku-copy. Lakini pamoja na yote hayo bado mpaka sasa haijatangazwa kama flash hii itaingia sokoni ila kwa mujibu wa Techradar, uwezekano wa flash hii kuingia sokoni ni mdogo sana kutokana na bei yake kukadiriwa kuwa kubwa sana.
Kwa sasa kama unataka kununua flash kutoka Western Digital yenye ukubwa wa TB 1 unaweza kuipata kwa dollar za marekani $400 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 920,000, sasa hadi hapo unaweza kuona bei ya TB 4 lazima itakuwa ni kubwa zaidi.
Kujua haya na mengine mengi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, pia unaweza kusoma ukurasa wetu wa CES 2019 ili kujua yote yanayoendelea kwenye mkutano wa CES unaofanyika huko Las Vegas nchini Marekani.