Kabla ya kuanza kujifunza jinsi ya kuflash simu za Tecno za Android ni vyema kujifunza maana ya baadhi ya maneno ili uweze kuelewa kinachofanyika hapa. Kwa kuanza twende tukaangalie nini maana ya neno Flash au fundi anaposema ana falsh simu ana kuwa na maana gani.
Kuflash simu ni nini ? kuflash simu ni neno linalotumiwa na mafundi simu likiwa na maana kuwa ni kitendo cha kurudisha au kurepair mfumo au sehemu ya mfumo wa uendeshaji kwa kuinstall copy ya mfumo huo ili kufanya simu yako kufanya kazi kama inavyotakiwa.
MAHITAJI MUHIMU
- USB Data Cable
- MT6577 USB VCOM Drivers (Win7/8 na Vista) – Download Hapa
- SP Flash Tool – Download Hapa
- Rom za Tecno – Download Hapa
- Kompyuta – Laptop au Desktop
HATUA
- Zima simu yako na utoe betri ya simu yako kama simu yako battery yake ni ya ndani hakikisha umezima simu yako kabisa.
- Fungua programu ya SP Flash Tool ambayo umedownload hapo awali.
- Fungua folder lenye programu hiyo kisha chagua SP Flash Tool.exe kisha bofya kitufe cha kulia kwenye mouse yako kisha bofya Run as Administrator.
- Kisha baada ya programu hiyo kufunguka bofya palipo andikwa Scatter Loading iliyopo upande wa kulia chini kidogo.
- Baada ya hapo chagua mahali ulipo hifadhi ROM ya simu yako kisha chagua file hilo na bofya Open, kumbuka mara nyingi file hili linakuwa na format ya .txt mfano (MT6577_Android_scatter_emmc.txt) kumbuka kuchagua file linaloendana na simu yako kwani ukikosea utaharibu simu yako.
- Weka tiki kwenye vyumba vyote isipo kuwa chumba kilicho andikwa Preloader, na DSP_bl hapa ni vyema kuwa makini mana unaweza kuharibu simu yako hakikisha unafuata hatua hizi sawa sawa.
- Baada ya hapo toa beattry kwenye simu yako kisha bofya YES kwenye programu ya SP Flash Tool.exe
- Kisha haraka chomeka simu yako kisha bofya vibovyezo hivi kwa pamoja vibonyezo vyote viwili vya sauti pamoja na kibonyezo cha kuwasha au power button.
Baada ya kufuata hatua zote hizo kwa makini utaona simu yako ikianza kupokea file kutoka kwenye kompyuta, subiri mpaka imalize na itakapo maliza kama ulifuata hatua sawa utaona meseji ikisema “You have successfully restored the Stock ROM”.
Kwa mafunzo zaidi ya teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.