Baada ya SanDisk kuleta Memory Card kubwa kuliko zote duniani, sasa kampuni ya teknolojia ya Kingston ya nchini marekani ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kuhifadhi data leo imetangaza rasmi kutoa flash drive kubwa kuliko zote duniani.
Flash hiyo yenye ukubwa wa Terabits 2 (TB2) imetengenezwa kwa teknolojia ya USB 3.1 Gen 1 performance ambayo inafanya flash hiyo kutuma data kwa kasi ya GB 5 kwa sekunde (5Gbps) hivyo kufanya flash hiyo kuwa ya kipekee zaidi na ya kwanza duniani kusoma kwa kasi ya namna hiyo.
Flash hiyo imetengenezwa kwa material ya zinc-alloy pamoja na metal casing ambayo husaidia flash hiyo kutopiga shoti pale inapokua imechomekwa kwenye kompyuta. Flash drive hiyo iliyopewa jina la DataTraveler Ultimate GT inategemewa kutoka mwezi February na itatoka kwa size mbili za TB 1 pamoja na TB 2 zote zikiwa na warranty ya miaka mitano kila moja.
Kampuni hiyo pia imesema itatoa huduma kwa wateja bure kabisa kwa miaka yote mitano pale mtu atakapo nunua flash hizo, kwa sasa kampuni ya kingstone bado haijatangaza bei ya flash drive hizo, lakini tegemea bei ya flash drive hizo kuwa juu kuanzia dollar za marekani $1,000 na kuendelea.