Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za Android basi ni wazi umeshawahi kusikia kuhusu neno Firmware, kama hujawahi kusikia basi kupitia makala hii nitaenda kukueleza nini maana ya Firmware hasa kwenye upande wa simu za Samsung.
Kwa kuanza basi ningependa kwanza ujue kuwa makala hii ni kwa ajili ya kujifunza, hivyo ni matumaini yangu itatumika vizuri kwa ajili ya kutoa elimu hasa kwa mtu yoyote anaye hitaji. Pia kumbuka kuflash simu ambayo sio yako ni kinyume na sheria, hivyo ni muhimu sana kufuata sheria unapotaka kufanya hivi.
TABLE OF CONTENTS
Nini Maana ya Firmware
Kwa maana ya darasani, Firmware ni programu endeshi ambayo inawekwa kwenye kifaa chochote cha kieletroniki kwa ajili ya kufanikisha kufikisha mawasiliano kwenye Hardware au kifaa chenyewe. Kwa upande wa simu, firmware ni mfumo unaotumiwa na kampuni husika kwenye simu yako ya Android, kwa mfano kama simu yako ni Samsung Galaxy S10, basi Firmware yake itakuwa Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa Samsung wa One UI.
SamFirm ni Nini
SamFirm hii ni programu ya mfumo wa Windows ambayo inatumika kuweza kudownload kwa haraka pamoja na kutafuta firmware za simu za Samsung. Programu hii ni bora sana kwa sababu inasaidia kupata Firmware halisi ya simu yako na pia utaweza kudownload firmware kwa haraka bila kukata kata.
Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kuflash simu za Samsung basi unaweza kutumia programu hii kuweza kudownload Firmware ya simu yako, Jinsi ya kutumia programu hii ni rahisi na unahitaji mambo ya fuatayo ili kusudu uweze kupata firmware ya simu yako kwa urahisi.
- Unahitaji kompyuta yenye mfumo wa Windows
- Unahitaji toleo jipya la programu ya SamFirm
- Unahitaji Internet pamoja na bando la kutosha
- Unahitaji kujua Model Number ya simu yako pamoja na mahali simu yako ilipo tengenezewa (Usijali nitakuonyesha jinsi ya kupata sehemu hizi zote).
Sasa kama unavyoweza kuona hayo ndio mahitaji ambayo unahoiitaji ili kusudi uweze kupata firmware ya simu yako ya Samsung kwa urahisi. Sasa ili kupata vitu hivi hebu twende hatua kwa hatua.
Download Programu ya SamFirm
Programu ya SamFirm inapatikana bure kabisa kwa mtu yoyote kudownload, unaweza kudownload programu hiyo kupitia hapo chini, kumbuka matoleo yote ya programu hiyo yanapatikana hapo chini ila ni muhimu kupakua toleo la 0.3.6 au 0.3.7.
- SamFirm_v0.3.1.zip
- SamFirm_v0.3.2.zip
- SamFirm_v0.3.3.zip
- SamFirm_v0.3.4.zip
- SamFirm_v0.3.5.zip
- SamFirm_v0.3.6.zip | Google Drive Link
- SamFirm_v0.3.7.zip
Jinsi ya Kutumia SamFirm
Baada ya kudownload extract mafile yaliyopo ndani ya file la zip, kisha ndani ya folder bofya sehemu ya samfirm.exe
Baada ya kubofya hapo endelea kwenye hatua inayofuata, kama ndani yake utaambiwa kuinstall programu ya Microsoft .NET Framework hakikisha unafanya hivyo. Baada ya kuwasha programu hiyo utaweza kuona muonekano kama huo hapo chini.
Baada ya hapo sasa ni wakati wa kutafuta Firmware ya simu yako, kwa kupitia mfano mimi nitaonyesha kutafuta firmware ya simu ya Galaxy S6.
- Hatua ya kwanza andika model number ya simu yako kwenye chumba cha Model, kama hujui model number ya simu yako unaweza kuipata kwa kuingia kwenye Settings > About Device.
- Baada ya hapo weka Region number kwenye sehemu ya Region, sehemu ambayo hii unaweza kuipata kwa uandika model ya simu yako kupitia tovuti hii.
- Baada ya hapo bofya Auto.
- Alfu bofya sehemu ya Check Update.
- Baada ya hapo subiri kidogo utaona maelezo yenye kuonyesha firmware ya simu yako imepatikana, baada ya hapo malizia kwa kubofya sehemu ya Download.
- Baada ya hapo chagua sehemu unayotaka kuhifadhi firmware kwenye kompyuta yako kisha moja kwa moja subiri imalize kudownload.
Baada ya hapo utakuwa uko tayari kuflash simu yako na unaweza kusoma hapa kujua hatua kwa hatua jinsi ya kuflash simu yako ya Samsung. Kumbuka njia hii ni kwa ajili ya simu za samsung pekee na haitofanya kazi kabisa kwenye simu nyingine.
Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha una subscribe kwenye YouTube channel yetu hapa ili kuweza kujifunza mambo mengi ya teknolojia. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku.