Download Mfumo wa Uendeshaji (Firmware) Simu za Infinix

Flash simu yako ya Infinix kwa kufuata hatua hizi (Download Firmware Hapa)
Firmware za Simu za Infinix Firmware za Simu za Infinix

Kama kwa namna yoyote umekuwa ukitafuta firmware kwaajili ya kuflash simu yako ya Infinix basi uko mahali sahihi. Kupitia makala hii nitaenda kukuelekeza jinsi ya kufalsh simu ya Infinix pamoja na link za kudownload firmware kwa ajili ya simu yako.

Kumbuka ni muhimu kuwa na kompyuta ili kuweza kufanya hatua hizi, pia ni vizuri kuwa na internet ya kutosha kwenye simu yako kwani file unazo kwenda kudownload ni kubwa hivyo ni muhimu kuwa na internet ya kutosha. Kama unataka kujua vifurushi vya bei nafuu kutoka kwenye mtandao wako unaweza kusoma hapa natumaini utapata kifurushi chenye kukidhi haja za matumizi yako.

Advertisement

Jinsi ya Kuflash Simu za Infinix

Kama unatumia simu ya Infinix yenye processor ya MediaTek ni muhimu kuwa na programu ya kuflash simu ya SP flash tool, unaweza kudownload programu hiyo hapa. Lakini pia kama unatumia simu ya Infinix yenye processor ya Qualcomm, unaweza kutumia programu ya Qualcomm Flash Image Loader. Mara nyingi simu nyingi za Infinix zinakuwa na processor ya MediaTek hivyo mara nyingi programu ya SP Flash Tool hutumika.

Lakini ni vyema kuwa makini na kuhakikisha ili usije kuharibu simu yako kwa kutumia programu ambayo haishauri. Kama tayari umesha download programu hizo kwenye kompyuta yako, sasa download drivers hizi za kuunganisha simu na kompyuta yako.

Baada ya hapo, Download Firmware unayo hitaji kupitia link hapo chini, hifadhi kwenye file moja na programu ya SP Flash Tool. Fungua (Unzip) programu ya SP Flash Tool kisha tafuta file lilo andikwa flashtool.exe, kisha bofya mara mbili kufungua programu hiyo.

Baada ya programu hiyo kufunguka, fungua (Unzip) firmware iliyopo kwenye file kisha rudi kwenye programu ya SP Flash Tool na sasa bofya kitufe cha Download kilichopo juu. Baada ya hapo bofya sehemu iliyoandikwa Scatter-loading na chagua firmware ya simu yako kisha bofya download.

Baada ya hapo chukua waya wa simu yako kisha chomeka simu yako kwenye kompyuta, baada ya hapo bofya kitufe chochote cha sauti cha simu yako na utaona hatua za kuflash simu yako zimeanza. N imuhimu kuhakikisha hatua hizi zinamaliza kwani hapo unaweza kuharibu simu yako. Baada ya kumaliza utaona tiki ya kijani.

Download Firmware za Simu za Infinix

Android 8.1 Infinix Firmware Flash Files

Android 7.0 Infinix Firmware Flash Files

Android 6.0 Infinix Firmware Flash Files

Android 5.1 Infinix Firmware Flash Files

Android 5.0 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.4.4 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.4 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.2.1 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.2 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.1.2 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.1 Infinix Firmware Flash Files

Android 4.0 Infinix Firmware Flash Files

Android 2.3.5 Infinix Firmware Flash Files

Android 2.3 Infinix Firmware Flash Files

Ni muhimu kuangalia model namba ya simu yako kabla ya kuchagua file unalotaka kudownload. Majina ya simu ni tofauti na model namba hivyo hakikisha una angalia model namba na sio jina la simu. Kama una maswali au maoni au kama kuna mahali umekwama tuandikie kupitia maoni hapo chini, pia unaweza kuandika jina la simu yako na tutaweka firmware yake kwenye ukurasa huu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use