Siku hizi kompyuta nyingi zinakuja na uwezo wa fingerprint moja kwa moja kwenye kompyuta yenyewe hivyo ni rahisi kuweza kutumia fingerprint kama sehemu ya ulinzi kwenye kompyuta hiyo, lakini je inakuaje kama kompyuta yako haina sehemu ya fingerprint, je unawezaje kutumia ulinzi wa namna hii kwenye kompyuta yako ingawa kompyuta yako haina sehemu ya sensor ya fingerprint..?
Sasa kupitia maujanja ya leo nitaenda kukuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kusaidia kuongeza ulinzi kwenye kompyuta yako kwa kutumia sehemu ya Fingerprint kwenye simu yako ya Android kufungua kompyuta yako. Njia hii ni rahisi sana na haitaji utaalamu wowote bali unahitaji kuwa na simu ya Android na kompyuta yoyote inayotumia mfumo wa uendeshaji wa Windows.
Kama unayo yote hayo basi unachohitaji kingine ni Internet ambayo na uhakika unayo kwani ndiyo iliyokuwezesha kusoma makala hii, kama tayari unayo simu ya android yenye sehemu ya Fingerprint na kompyuta yoyote inayotumia Windows pamoja na kifurushi cha Internet cha angalu MB 200 basi uko tayari kujifunza maujanja haya na bila kukupotezea muda twende tukajifunze moja kwa moja.
Kwa kuanza unatakiwa kupakua programu ya Android ya Remote Fingerprint Unlock ambayo unaweza kuipakua kwa kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye soko la Play Store ili ku-install programu hiyo.
Remote Fingerprint Unlock
Baada ya kuinstall App hiyo kwenye simu yako sasa huko tayari kuendelea kwenye hatua ya pili, hatua hii sasa unahitaji kufungua kompyuta yako na ingia kwenye makala hii kisha pakua programu maalum ya Windows kwaajili ya kuwezesha sehemu ya fingerprint kwenye kompyuta yako. Kumbuka chagua Bits zinazofanana na kompyuta yako yaani x64 kwa kompyuta yenye 64 bits na x32 bits kwa kompyuta yenye 32 bits.
Kwa wale wenye kompyuta zenye 64 bits unaweza kuchagua programu yoyote iwe ya x64 au x32, ili kuweza kujua unaweza kuangalia mbele ya jina la programu kujua ni aina gani ya programu unapakua. Unaweza kupakua programu hiyo ya Windows HAPA. Baada ya kupakua programu hiyo Unzip programu hiyo kisha Install kwenye kompyuta yako na baada ya kuinstall endelea kwa kuweka kompyuta yako kwenye Lock Screen kisha chukua simu yako na washa programu ya Remote Fingerprint Unlock.
Baada ya kuwasha programu hiyo bofya sehemu ya mishale mitatu kwa juu upande wa kushoto kisha fungua menu na chagua sehemu ya Scan, huku kompyuta yako iko kwenye Lock screen bofya sehemu ya Search iliyoko chini upande wa kulia. Baada ya hapo kama kompyuta yako iko kwenye Lock Screen utaweza kuona jina la kompyuta yako kwenye App uliopakua hapo awali.
Baada ya kuona jina la kompyuta yako kutokea bofya jina hilo kisha bofya kwenye sehemu ya Add Account weka kidole chako kwenye sehemu ya fingerprint kwenye simu yako kisha maandishi yakiwa ya blue andika jina la ambalo ungependa kutumia pia andika na password baada ya hapo maliza kwa kubonyeza Save kumbuk yote haya unafanya huku kompyuta yako ikiwa iko kwenye Lock Screen hakikisha inaendelea kuwa kwenye hali hiyo kwa kipindi chote unapafanya hatua hizi.
Baada ya kubofya Save shilia kwenye jina la Kompyuta yako kisha litabadilika na kuwa na maandishi selected, baada ya hapo bofya sehemu ya menu kisha chagua sehemu ya unlock na baada ya hapo weka kidole chako kwenye sehemu ya fingerprint ya simu yako na utaona kompyuta yako imefunguka.
Baada ya kufuata hatua zote hizo hapo utakuwa umeweza kuweka ulinzi wa fingerprint kwenye kompyuta yako kwa kutumia sehemu ya fingerprint ya simu yako. Kama utakuwa umekwama kwa namna yoyote endelea kutembelea Youtube ya Tanzania Tech tutaweka video ya hatua kwa hatua jinsi ya kufanya hatua hizi.