Snapchat ni moja kati ya mtandao ambao ulikuwa ikitumiwa na watu wengi sana miaka kadhaa iliyopita, hadi hapo Instagram pamoja na Facebook zilipo anza kunakili baadhi ya sehemu zilizopo kwenye mtandao huo.
Lakini japo kuwa instagram na Facebook zilifanikiwa kunakili baadhi ya sehemu ikiwa pamoja na kuchukua watumiaji wa mtandao huo wa Snapchat, lakini bado mtandao huo umeendelea kuwepo na kufanyiwa maboresho tofauti na watu wengi walivyofikiria labda mtandao huo ungeweza kufa.
Sasa siku za karibuni mtandao wa Snapchat umeonekana kuanza kutumiwa tena na watu wengi zaidi kutokana na aina mpya za Filter ambazo zimeongezwa kwenye programu hiyo. Filter hizo ni pamoja na zile ambazo zinaweza kubadilisha sura ya mwanamke kuwa kama ya mwanaume na sura ya mwanaume kuwa ya kama ya mwanamke.
Filter hizo zimeonekana kutumiwa na watu wengi maarufu huku wengi zaidi wakichukua picha hizo na kuzituma kwenye akaunti zao za Instagram pamoja na Twitter. Moja kati ya watu ambao wameonekana kufurahia Filter hizo ni pamoja na mwanamuziki, muigizaji na mwandishi Miley Cyrus ambaye alituma picha yake kama mwanaume kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Umm why did Snapchat turn me into @joejonas? It’s our brows? pic.twitter.com/OlXgiRL5va
— Miley Cyrus (@MileyCyrus) May 12, 2019
Kwa mujibu ya tovuti ya Similarweb, App ya Snapchat imeonekana kupakuliwa na watu wengi zaidi huku ikishika namba moja kwenye soko la Play Store kwenye nchi ya Marekani kutoka namba 5 ambapo ilikuwa awali.
Hata hivyo watumiaji wengi hatumi programu hiyo kwaajili ya kuweka picha kwenye mtandao huo, bali wengi wao hutumia kama sehemu ya kutengeneza picha kupitia Filter mbalimbali na baada kuchukua picha hizo na kuziweka kwenye Stories za mitandao ya Instagram pamoja na Facebook.
Kwa sasa kama unataka kujaribu Filter hizo mpya tayari zinapatikana kwa watumiaji wote duniani na unaweza kupakua app ya Snapcha na kujaribu sehemu hizo. Unaweza kupakua app ya Snapchat kwa kubofya hapo chini.
Kwa habari zaidi za Teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, tutakupa habari mpya za teknolojia kila siku na kila saa.