Wakati dunia ikiwa imepata fundisho kubwa la kuhakikisha biashara zote zinakuwa mtandaoni, hivi karibuni klabu ya soka ya FC Barcelona nayo imeonyesha kuwa fundisho hilo sio kwa biashara za kawaida tu bali hata klabu za soka nazo zinahitaji kuwa mtandaoni kwa kiasi kikubwa.
Klabu hiyo kubwa ya soka duniani, hivi karibuni imetangaza ujio wa mtandao wake wa Barca TV+ mtandao utakao kuwa kama mtandao wa Netflix lakini kwa ajili ya soka. Kwa mujibu wa tovuti ya Variety, Barca TV+ ni mtandao ambao utakuwa una onyesha makala mbalimbali za soka ikiwa pamoja na wasifu wa wacheza mbalimbali waliopo na waliopita kwenye klabu hiyo.
Mbali ya kuonyesha wasifu wa wachezaji, pia utaweza kuona makala za historia ya klabu hiyo ya soka pamoja na mambo mengine mengi ambayo yatakufanya ufahamu zaidi klabu hiyo. Kwa sasa, kuna video fupi kwenye tovuti hiyo ambayo watazamaji wanaweza kutazama video hizo bure kwa kusajili bila kulipia. Lakini pia, zipo video ambazo zipo kwaajili ya watumiaji wa kulipia.
Hivi karibuni hapa nchini Tanzania, klabu ya soka ya Simba SC nayo ilizindua tovuti yake ambayo itakuwa inatoa habari mbalimbali kuhusu klabu hiyo ikiwa pamoja na matokeo ya michezo mbalimbali iiyochezwa na klabu hiyo hapa nchini Tanzania na hata nje ya nchi.
Kama wewe ni mpenzi wa klabu ya soka ya FC Barcelona, basi unaweza kujisajili kwenye tovuti ya Barca TV+ kupitia link hapo chini.